loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafugaji nyuki marufuku kuvuna asali kwa moto

WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imepiga marufuku wafugaji nyuki kuvuna asali kwa njia ya kuchoma moto na kuwateketeza nyuki.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani Pemba, Suleiman Ali Makame aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na watu wanaovuna asali kwa kuteketeza nyuki.

Dk Ussi alisema ni uharibifu wa mazingira kwa wavunaji asali kuchoma moto nyuki wakati wakiwa katika harakati za kugema asali. Alisema matukio kama hayo athari zake kubwa zimeonekana ikiwemo baadhi ya misitu kuteketea kutokana na tabia ya wafugaji nyuki kuchoma moto wakati wakigema asali.

“Haikubaliki, ni kitendo cha uharibifu wa mazingira wakati nyuki akiwa anahitajika kwa ajili ya kuzalisha asali watu wanawateketeza kwa kuwachoma moto,” alisema Dk Ussi.

Alisema tayari wameanza kutoa mafunzo mbali mbali kwa wafugaji nyuki juu ya njia sahihi za kuvuna asali bila ya kusababisha madhara ikiwamo kuua nyuki. Kwa mfano, alisema jumla ya wafugaji nyuki 700 wamepatiwa elimu ambayo itawawezesha kuvuna asali kwa njia za kisasa bila ya kuharibu mazingira.

Aidha, alisema jumla ya vikundi 250 vimepatiwa mizinga ya kibiashara kwa ajili ya ufugaji nyuki.

“Vikundi vya wafugaji asali vingi tumevipatia mafunzo juu ya kuvuna asali kwa kuzingatia mazingira na uhifadhi wake......sioni sababu ya kuchoma nyuki wakati wa kuvuna asali,” alisema.

Dk Ussi aliwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba shughuli za kufuga nyuki kwa ajili ya kuzalisha asali imeanza kuleta matunda mazuri kwa wananchi wa Unguja na Pemba ikiwamo kujitokeza vikundi

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi