loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ajali ya meli ya mafuta Mt Ukombozi yaundiwa tume

WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji imeunda Tume kuchunguza ajali ya meli ya mafuta ya Mt Ukombozi iliyotokea miezi miwili iliyopita katika Bandari ya Wesha Pemba na kuua wafanyakazi wake watatu.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohamed Ahmada wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kufahamu tume iliyoundwa wajumbe wake na majukumu yake kwa ujumla.

Ahmada alisema ni kweli serikali imeunda tume ya kuchunguza kuungua kwa meli ya mafuta ya MT Ukombozi ambayo ilisababisha vifo vya mabaharia watatu. Alisema uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kujitokeza kwa hitilafu za umeme na mlipuko wa gesi.

“Huo ni uchunguzi wa awali katika tukio la mripuko wa meli ya Mt Ukombozi.....sasa tumeunda tume rasmi kujuwa chanzo cha ajali hiyo,” alisema Naibu Waziri.

Aliwataja wajumbe wa tume hiyo ni Jaji Shaaban Ramadhan Abdalla, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyefahamika kwa jina moja la Fatuma, Kepteni Makame Hassan Ameir wa Shirika la Bandari la Zanzibar na Abdalla Kombo ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini.

Katika timu ya uchunguzi wapo, wajumbe wataalamu kutoka Tanzania Bara kutoka taasisi za vyombo vya baharini na meli. Ahmada alisema tume hiyo inatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha taarifa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

“Kazi ya uchunguzi wa kitaalamu imeanza ikiwahusisha wajumbe kutoka Zanzibar pamoja na wenzetu kutoka Tanzania Bara.....tunatarajia kuchukuwa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo na taarifa yake itatangazwa kwa wananchi,” alisema Ahmada.

Meli ya Mt Ukombozi iliungua moto huko katika Bandari ya Wesha Pemba baada ya kujitokeza hitilafu za umeme huku wafanyakazi wa meli hiyo wakiwa katika harakati za usafi katika sehemu ya moja ya chumba cha injini.

Ajali hiyo ilisababisha kujeruhiwa vibaya kwa mabaharia wake watatu kwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na baadaye kufariki. Waliokufa ni Ali Juma (54), Hafidh Silima Kona (25) na Issa Daud Omar (30).

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi