loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majukwaa sekta ya uziduaji gesi yaendelezwe -Zambi

MKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amezitaka mamlaka za uongozi mkoani humo ambazo zina sekta ya uziduaji wa gesi kuhakikisha wanaendeleza majukwaa yaliyoanzishwa ili kuleta uelewa, ushirikiano na kuendeleza uchumi wa mkoa.

Kauli hiyo aliitoa juzi katika ufunguzi wa jukwaa la mkoa la wadau wa sekta ya uziduaji wa gesi asili lililoshirikisha viongozi wa mkoa, dini na waragibishi lililofanyika mjini Kilwa Masoko wilayani Kilwa. Jukwaa hilo limeelezwa kuwa lina lengo la kuimarisha ushiriki wa wananchi, uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mapato ya tozo ya huduma katika sekta ya uziduaji wa gesi asilia na mafuta.

Kwa sasa Mkoa wa Lindi unatoa gesi asilia katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa na kuna mpango wa kuanzisha usindikaji gesi (LNG), Wilaya ya Lindi.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kutokana na majukwaa hayo, kumekuwepo na uwazi na amani katika matumizi ya tozo, hivyo ni wajibu wa watendaji wa serikali kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Lindi (LANGO) wa kuhakikisha kuna jukwaa la mawasiliano kwa lengo la kuongeza tija.

Lango ambao wanaendesha mradi wa uwajibikaji pamoja na kuanzishwa majukwaa ngazi ya kijiji, wilaya na mkoa pia umetoa elimu kwa viongozi wa serikali, wananchi, waandishi wa habari na waragibishi kwa lengo la kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo. Kutokana na ufuatiliaji huo kwa sasa halmashauri ya wilaya ya Kilwa imeweza kupeleka kisiwa cha Songosongo asilimia 20 ya asilimia 0.3 ya tozo wanayopelekewa na waziduaji wa gesi kisiwani humo. Aidha, kisiwa hicho kwa sasa kimekuwa na ufuatiliaji wa fedha zinazopelekwa kwao kwa ajili ya mahitaji. Zambi pamoja na kushukuru Taasisi ya OSIEA kwa kufadhili mradi huo kupitia Lango, pia ametaka watendaji kubainisha mafanikio chanya yanayoletwa na sekta ya uziduaji na kuhakikisha wanafuatilia fedha kwa lengo la kuhakikisha miradi ya kimkakati inabuniwa na kutekelezwa ili kupanua wigo wa vyanzo vya mapato. Akizungumzia ushiriki wao katika kuelimisha wananchi Ofisa Miradi wa Lango, Aina Pero alisema kwa miaka takribani mitano wamekuwa wakiendesha miradi mbalimbali kisiwani Songosongo na Lindi katika sekta ya uziduaji. Alisema kuwapo kwa majukwaa ambapo wadau wanakutana na kubadilisha mawazo na pia kutengeneza maelewano katika mapato na matumizi yanayotokana na tozo za uziduaji gesi, kumesababisha wananchi kuwa na sauti katika uwekezaji huo.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kilwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi