loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pwani wakusanya kodi ya Sh bil 147

MKOA wa Pwani umefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 147 kutokana na kodi mbalimbali katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu Tano. Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo wakati wa kikao cha mashauriano kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa huo.

Ndikilo alisema kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2015 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa huo walikusanya kiasi cha Sh bilioni 64.9.

“Fedha hizo za kodi zilitokana na kodi za Vat, income tax, paye ukiondoa kodi ya forodha nakushika nafasi ya 12 kati ya mikoa 30 ya kikodi nchini,” alisema Ndikilo.

Alisema Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miaka minne iliyopita kwa kigezo cha ukusanyaji wa kodi ulikuwa chini sana na ulikuwa hautajwi lakini katika serikali hii mkoa umepiga hatua kubwa.

“Tunaomba kupewa sehemu ya Ranchi ya Taifa Narco ukubwa wa ekari 6,000 kwenye eneo la Bandari Kavu ya Kwala Kibaha Vijijini ili kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuegesha magari, biashara, makazi, mahoteli na maghala, viwanda,” alisema Ndikilo.

Aidha, alisema Narco wana eneo lenye ukubwa wa ekari 30,000 hivyo endapo watapata eneo hilo ili liwe la uwekezaji kwani ni karibu na Reli ya Kati, Reli ya Kisasa, Reli ya Tazara, sehemu ya kupokea umeme kutoka Bwawa la Nyerere Rufiji, jirani Bandari ya Dar es Salaam, chanzo cha maji ya Dawasa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Abdala Ndauka alisema changamoto mojawapo ni baadhi ya taasisi za zinazohusika na vibali kutumia nguvu badala ya kutoa elimu.

Naye mfanyabiashara wa viwanda vya kokoto, Ally Murad alisema wanatumia gharama kubwa ya umeme wa jenereta wanaotumia kutokana na kutokuwa na umeme wa Tanesco hivyo wanaomba kupatiwa umeme.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi