loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kigogo wa maji Misungwi asimamishwa kazi

NAIBU Waziri wa Maji, Juma Aweso amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Wilaya ya Misungwi (MIWASA), Charles Kampuni, baada ya kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Old Misungwi.

Aweso alisema sababu nyingine ya kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo kunatokana na kusuasua kwa mradi wa maji wa Ihelehe uliopo katika Kijiji cha Nyamgo’mango.

Alisema mradi huo ni wa muda mrefu tangu mwaka 2014 lakini mpaka leo haujaweza kukamilika huku wakazi wa Misungwi wakikabiliwa na kero ya maji kwa muda mrefu.

Mradi wa Ihelele upo chini ya Mkandarasi Shanxi Construction Engineering Cooperation and Mineral Company na mpaka sasa serikali imeshatoa Sh bilioni 1.2 Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga amemuomba Naibu Waziri Aweso kuwasaidia katika ujenzi wa visima katika kata ya Kijima, Isesa, Fella na Igenga ili wakazi wa Misungwi wapate maji.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amemuagiza ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi