loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri ambana mkandarasi upanuzi kituo cha umeme

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amekagua maendeleo ya upanuzi wa kituo cha kupoza umeme Bulyanhulu, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi husika ifi kapo Mei, 2020.

Akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa pamoja na wataalamu kutoka wizarani, Tanesco na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Waziri pia alimwagiza Meneja wa Tanesco mkoani humo kumsimamia mkandarasi ili akamilishe kazi kwa wakati na viwango stahiki.

“Hii ni kazi muhimu sana hivyo lazima ikamilike kwa wakati. Tunapanua kituo hiki ili kukiongezea uwezo kutoka megawati 16 za sasa hadi kufikia megawati 51. Ujenzi ni mkubwa maana utahusisha pamoja na mambo mengine, kujenga njia ya kusafirisha umeme umbali wa kilomita 57 kutoka Bulyanhulu hadi Geita,” alisema.

Aidha, alieleza kuwa, ujenzi utakapokamilika, kituo hicho kitasaidia kufua na kupitisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 unaotoka Shinyanga kwenda hadi Geita ambako pia kunajengwa kituo kingine kikubwa cha megawati 100.

Akifafanua zaidi, waziri alisema ujenzi wa kituo cha Geita pamoja na upanuzi wa kituo cha Bulyanhulu, gharama yake ni takribani dola za Marekani milioni 23 na kwamba mradi unahusisha pia kupeleka umeme kwenye vijiji 10 kutoka Bulyanhulu kupitia Busanda hadi Buseresere.

Awali, waziri alitembelea kijiji cha Igunda wilayani humo, ambapo aliwasha rasmi umeme. Pia alitembelea Kijiji cha Ntobo, Kata ya Msalala na kuwaeleza wananchi kuwa umeme utafikishwa katika kijiji hicho hivi karibuni.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Kahama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi