loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maonesho ndege vita, makomandoo yatia fora

MOJA ya mambo yaliyovutia na kushangiliwa sana na wananchi kwenye sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana na miaka 57 ya Jamhuri, ni miondoko ya ndege vita na onesho la makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, zilipambwa na nyimbo, ngoma za jadi na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kutoka Mkoa wa Mwanza na mikoa mingine nchini.

Ndege vita zilikuwa zikipita kwa mwendokasi na mbwembwe nyingi, hali iliyosababisha wanan- Na Nashon Kennedy, Mwanza WAKAZI wa Mkoa wa Mwanza wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa uamuzi wake wa kuruhusu sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara kufanyika kitaifa kwa mara ya Kanda ya Ziwa na mkoani Mwanza.

Wamesema hatua hiyo imewaunganisha Watanzania na kuimarisha umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa. Waliyasema hayo jana, walipozungumza na gazeti hili kuhusu furaha waliyo nayo sanjari na kutoa pongezi kwa Rais John Magufuli, kwa mapenzi makubwa aliyo nayo kwa Watanzania kwa ujumla.

Sherehe hizo za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na 57 ya Jamhuri, zilifanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika Kanda ya Ziwa na mkoa huo.

“Kwa namna ya kipekee nimpongeze Rais John Magufuli, ameniwezesha kwa mara ya kwanza kushuhudia miaka 58 ya Uhuru, sherehe ambazo sijawahi kuzishuhudia moja kwa moja tangu nizaliwe,” alisema Getrude Ntemi, mkazi wa Bwiru jijini Mwanza.

Naye Joseph Bangilana alisema sherehe za Uhuru za mwaka huu, zimetia fora huku akitoa ushuhuda wa kutoka nyumbani saa 10 alfajiri ili kuwahi sehemu ya kukaa ili awe mmoja wa wahudhuriaji na afaidi uhondo wa maadhimisho hayo, yaliyopambwa na shughuli mbali mbali kama gwaride, nyimbo, maonesho ya ndege na halaiki.

“Nimefurahishwa sana na gwaride la Jeshi letu hasa zile ndege za kivita, mpangilio wa sherehe hizi umekwenda vizuri, wananchi tumeonyesha ustaarabu mkubwa na amani imetawala,” alisema.

Mkazi wa Bukara Kishiri wilayani Nyamagana, Esau Malibwa alisema sherehe za mwaka huu, zimekuwa na tofauti na zile za miaka ya nyuma kwa sababu zimewaleta na kuwaunganisha viongozi wa kitaifa na wale wa vyama vya siasa. Makamu Mwenyekiti wa ADC Taifa, Shaaban Itutu alisema maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru ni tafsiri ya maendeleo makubwa, ambayo yamefanyika katika sekta za afya, elimu na miundombinu.

Lakini, aliiomba serikali itilie mkazo kwenye uboreshaji wa viwanda, ambavyo vingi vya viwanda vilivyoanzishwa wakati nchi inapata Uhuru vimekufa na havifanyi kazi. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (Namba Tatu) alisema maadhimisho ya mwaka huu, ambayo yamefana ni uthibitisho kwa Watanzania kuwa Rais Magufuli anafanya kazi ya kutukuka. Aliwaomba Watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini, waendeee kumuombea.

“Maendeleo makubwa haya tunayoyashuhudia leo asingekuwa Rais Magufuli tusingeyaona, tumuunge mkono kwa kufanya kazi, na sisi CCM Mkoa wa Mara tutaendelea kumuunga mkono hatutamuangusha,” alisema Kiboye.

Na Nashon Kennedy, Mwanza MAADHIMISHO ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na 57 ya Jamhuri ya Tanzania, ambayo kwa mara ya kwanza mwaka huu yamefanyika kitaifa Kanda ya Ziwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, yamefana kwa maelfu ya wakazi wa mikoa ya kanda hiyo kuhudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na 57 ya Jamhuri zilifanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika Kanda ya Ziwa na mkoa huo.

Kwa muda mrefu, zimekuwa zikifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mahali ambako Desemba 9, 1961 bendera ya Tanganyika ilipandishwa kuipa Uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Uingereza. Aidha, sherehe hizo zimewahi kufanyika mkoani Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri, Desemba 9, 2017 wakati wa kuadhimisha sherehe za miaka 56.

Kwa sasa, Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi baada ya serikali kuhamia rasmi. Sherehe za jana zilianza kwa maelfu ya wakazi wa mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa na wale wa mikoa jirani kuwasili uwanjani saa 10:30 alfajiri. Hata hivyo, ilipofika saa 12:07 asubuhi walianza kuzuiliwa katika barabara ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza, ambako ndiko ulipo Uwanja wa CCM Kirumba.

Uwanja wa CCM Kirumba uliripuka kwa furaha baada ya Rais John Magufuli kuwasili uwanjani saa 3:13 na kuzunguka uwanja na kushangliwa na maelfu ya wananchi na kupigiwa mizinga 21. Aidha, uliimbwa wimbo wa Taifa wa Tanzania na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Baadaye Rais Magufuli alikagua gwaride hilo kwa mwendo pole, akisindikizwa na wimbo wa Tanzania ulioimbwa na gwaride la kijeshi.

Awali, sherehe hizo zilianza kwa viongozi wastaafu waliowasili uwanjani wakiongozwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mawaziri wakuu wastaafu waliongozana na wake zao waliwasili, wa kwanza akiwa Frederick Sumaye, Mizengo Pinda, Edward Lowassa na John Malecela.

Mbali na hao, walikuwapo viongozi wengine wa serikali zote mbili, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwamo Rais Dk Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Pia walikuwapo Spika wa Bunge, Job Ndugai, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Othman Makungu, maspika wastaafu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge na watendaji wa serikali. chi uwanjani hapo kulipuka kwa furaha na vifijo.

Ndege vita tatu moja ikiwa kushoto, nyingine kulia na nyingine juu kidogo ya hizo mbili, zilipita kwa mwendokasi mbele ya Rais John Magufuli, viongozi mbalimbali na maelfu ya na wananchi waliofika uwanjani hapo. Dakika kama tatu baadae ikapita ndege vita moja ikiwa kasi, baadae zikafuata ndege vita zingine tatu zikipita kwa mwendokasi na mbwembwe nyingi kwa mtindo wa kivta.

Furaha ya wananchi uwanjani hapo, ililipuka tena baada ya ndege nyingine vita kupita kwa kasi, kwa mtindo ulioelezwa kuwa mtoroko yaani wa kumtoroka adui. Hatimaye ikapita ndege vita ya mwisho kwa mwendo wa kawaida, huku ikifanya madoido, yaliyoelezwa kuwa ni kutoa heshima kwa Rais.

Furaha ya ndege vita ilifuatiwa na uhondo mwingine wa Kwata ya kimyakimya, iliyofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Miongoni mwa mambo walioonesha kwenye kwata hiyo ni uwezo wao wa kucheza na silaha hususani bunduki, huku wakigeuka kwa staili ya kuvutia, ikiwemo mbinu ya kumlinda kiongozi wao huku wakiwa wametengeza duara. Kabla ya hayo yote, kulitanguliwa na gwaride la mwendo pole na mwendokasi la majeshi ya ulinzi na usalama, wakitoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli.

Mambo yakawa moto tena, baada ya makomandoo nao kuonesha mbinu za kijeshi za kumuokoa kiongozi muhimu, aliyetekwa na kushikiliwa na maadui. Helikopta ya kijeshi ilionekana angani na muda mfupi ilifika eneo la tukio la kubuniwa, yaani ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, ikimleta kiongozi wa makomando aliyeongoza kazi ya uokoaji.

Komandoo huyo kiongozi na makomando wengine waliokuwa naye, walishuka kwa kutumia kamba kutoka kwenye helikopta hiyo iliyoganda angani. Baada ya makomandoo hao kushuka, waliungana na makomandoo wenzao waliokuwepo ardhini. Kutokana na umahiri wao, walifanikiwa kuwadhibiti maadui kwa kutumia medani za kivita, magari ya kijeshi na helikopta ya jeshi.

Kwa kutumia akili na maarifa ya kivita, walimuokoa kiongozi huyo muhimu, aliyetekwa na kushikiliwa na maadui. Makomandoo hao waliondoka na kiongozi huyo na muda mfupi baadaye ikapita helikopta ya kijeshi, kutoa heshima kwa Rais. Maonesho hayo yaliwafanya wananchi, kushangilia muda wote huku wakisifu ushupavu wa askari hao. Mbali na maonesho hayo ya ndege vita na makomandoo, walinzi wa jadi kutoka kabila la Wasukuma, nao waliingia kuonesha namna wanavyofanya ulinzi wa sungusungu.

Wasukuma walianzisha ulinzi huo mwaka 1982 mkoani Shinyanga na mwaka mmoja baadaye ulinzi huo wa jadi, ulienea kanda nzima ya Ziwa. Burudani hizo zilifanya maelfu ya wananchi uwanjani, kusherehekea vema sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Wengine maelfu walikuwa nje na wengine katika uwanja jirani wa Furahisha na kote huko waliwekewa televisheni kubwa kufuatilia matukio yote. Kwaya ya Kanisa la AIC iliimba wimbo maalumu wa kudumisha amani Tanzania.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi