loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiswahili kufundishwa rasmi Uganda Januari

SHULE zote za msingi nchini Uganda, Januari mwakani zitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili na baadae kufanya mitihani kwa lugha hiyo.

Hatua hiyo imeelezwa ni mkakati wa nchi hiyo, kutaka kujitanua katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuona nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo na nje ya jumuiya zimeitangaza lugha hiyo kuwa rasmi na kuwekwa kwenye mitaala. Mbali na hatua hiyo, Uganda pia imeanzisha Baraza la Kiswahili, huku kikianza kusambaa kwa kasi mashuleni.

Nchi nyingine za Afrika Mashariki ambazo zinakitambua Kiswahili kama lugha rasmi ya taifa ni Tanzania, Kenya na Rwanda, huku Burundi na Sudan Kusini zikiingiza lugha hiyo adhimu katika mitaala yake ya shule. Wizara ya Elimu Uganda imesema nchi hiyo imejiandaa kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili shuleni, baada ya kufanyika majaribio na kwamba itaanza kufundishwa kuanzia darasa la nne mpaka la saba.

Kamishna Msaidizi wa Elimu ya Msingi Uganda, Dk Tony Mukasa alisema hayo wakati wa mkutano wa maofisa tawala uliofanyika juzi nchini humo.Alisema tayari wameshambaza vitabu vya Kiswahili shuleni, huku walimu wakiwa wamepata mafunzo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

“Lengo ni kukukifanya Kiswahili kuwa lugha ya pili ya taifa kutokana na kuwa inatumika kwa kiasi kikubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema.

Dk Mukasa alisema alitahadharisha kuwa shule ambazo hazitatekeleza sera hiyo, zitapata shida miaka mitatu ijayo, kwani wizara inatarajia kuwa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi utakaoandikwa kwa Kiswahili.

“Katika siku za baadaye tunatarajia kukifanya Kiswahili lugha itakayofanyiwa mtihani na kusimamiwa na Bodi ya Taifa ya Mitihani Uganda katika elimu ya msingi,” alisema.

Miaka ya hivi karibuni, serikali Uganda iliaidi kuanza kutekeleza utoaji mafunzo ya lugha hiyo shuleni, lakini ilichukua muda kutokana na kutokuwa na sera maalum ya maendeleo ya lugha hiyo.

Mwakilishi wa Chama cha Walimu Uganda na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kisugu iliyopo Kampala, James Jjuko, alisema hajui mipango hiyo ya serikali na kwamba shuleni kwake wana vitabu vya lugha ya Kiswahili, lakini hawana mwalimu wa kufundisha lugha hiyo. Kauli hiyo iliungwa mkono na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Triple P, Plan Virginia, aliyesema serikali imekuja na sera hiyo bila mpangilio hivyo inaweza kusababisha migogoro.

Septemba mwaka huu serikali ilipitisha kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Kiswahili Uganda, ikiwa ni maandalizi ya a kutangazwa kuwa lugha rasmi ya pili ya taifa. Akizungumzia hatua hiyo ya Uganda, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita), Dk Selemani Sewange, alisema ni takwa la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuzitaka nchi wanachama kutambua Kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa. Alisema itifaki ya Kamisheni ya Kiswahili EAC, inasema kila nchi inatakiwa kuwa na Baraza la Kiswahili na baadaye lugha hiyo kupanuliwa kwa kufundishwa shuleni.

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesisitiza ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi