loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mabondia Tanzania wapewa somo

MABONDIA Watanzania wametakiwa kujiaandaa vyema kabla ya kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa.

Rai hiyo imetolewa baada ya mabondia wa Tanzania, Swedi Mohamed na Suleiman Said kupigwa kwa Knockout (KO) katika mapambano ya utangulizi kabla ya pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz na Anthony Joshua lililofanyika nchini Saudi Arabia juzi.

Akizungumzia mapambano hayo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBRC), Yahya Poli alisema mabondia ni vema kujiandaa kabla ya kukubali pambano kuepuka fedheha ya kupata kipigo.

“Kupigwa katika ndondi ni kitu cha kawaida lakini tunaangalia umepigwa pigwaje, hivyo nawashauri mabondia kujiandaa vema kabla ya kukubali pambano kwani kufanya hivyo kunawajengea heshima,” alisema Poli.

Swedi Mohamed alichapwa na Ivan ‘Hopey’ Price wa Uingereza katika raundi ya tatu kwenye pambalo la uzito wa Super Bantam na Suleiman Said alipigwa hadi akakaa raundi ya kwanza na Mmarekani Diego Pacheco katika uzito wa kati Katika usiku huo wa masumbwi Anthony Joshua alifanikiwa kurejesha mataji yake ya WBA, WBO, IBO na IBF baada ya kumshinda kwa pointi za majaji, 118-110 mara mbili na 119-109, Andy Ruiz.

Joshua alipokonywa mataji yake ya WBA, WBO na IBF baada ya kupigwa na Ruiz kwa Knockout (KO) raundi ya saba katika pambano lililofanyika Juni mwaka huu ukumbi Madison Square, New York, Marekani.

Ikumbukwe juzi bondia mwingine, Mtanzania, Bruno Tarimo ‘Vifua Viwili’ alifanikiwa kutwaa taji la IBF International uzito wa Super Feather baada ya kumshinda kwa pointi mwenyeji, Nathaniel May ukumbi wa ICC Exhibition Centre mjini Sydney, Australia.

Bondia huyo mzaliwa wa Rombo, mkoani Kilimanjaro alimzidi mpinzani wake kwenye pambano hilo la raundi 10 na haikuwa ajabu kutangazwa mshindi jana.

Hilo lilikuwa pambano la 28 kwa Tarimo tangu ajiunge na ngumi za kulipwa Desemba 25, mwaka 2013 akiwa ameshinda mara 25, mara tano kwa KO, amepigwa mara mbili zote kwa KO na droo moja.

KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi