loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanasiasa, wasomi waunga mkono ujenzi taifa moja

WASOMI na wanasiasa wakongwe nchini wameyaelezea maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru, yaliyofanyika jijini Mwanza juzi, kuwa ya kihistoria na kwamba yametoa mwelekeo mzuri wa kulijenga taifa bila kujali itikadi.

Aidha, wamevitaka vyama vya upinzani nchini, kuendelea kushiriki vyema katika matukio ya kitaifa, kwa kuwa siku zote maendeleo ya nchi hayana chama.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Dar es Salaam, Spika mstaafu Pius Msekwa alisema muungano wa upinzani na serikali katika maadhimisho hayo ya uhuru, ulifurahisha na kuonesha umoja wa kitaifa katika kujenga nchi.

“Kwa kweli hali ya jana (juzi) ilifurahisha na kupendeza, ilionesha katika taifa letu hakuna mpasuko wa kudumu wala usiotibika,” alisema Msekwa.

Alisema tangu mwaka 2015 vyama vya upinzani nchini, vilisusa kushiriki katika matukio yote ya kitaifa, baada ya kushindwa kwenye uchaguzi, lakini katika maadhimisho ya mwaka huu ya uhuru walithibitisha kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Alisema akiwa mwanasiasa mkongwe, anawashauri viongozi wa vyama vya upinzani nchini, kuacha kuingiza hasira kwenye masuala yanayohusu taifa, bali matukio yote ya kitaifa wayaangalie kwa macho ya kitaifa zaidi.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (Ruco), Profesa Gaundence Mpangala amesema katika utawala wa Rais Dk John Magufuli, kwa miaka miwili sherehe za kitaifa alizifuta na fedha kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo.

“Sasa kutokana na hatua hiyo, maadhimisho haya kufanyika yamewavutia wengi kushiriki. Hata hivyo hakuna sababu ya upinzani kutoshiriki katika shughuli hizi za kitaifa. Uhuru wa nchi ni tukio muhimu katika taifa halina chama,” alifafanua.

Alisema inaeleweka endapo wapinzani watasusia matukio kama uchaguzi, hasa pale wanapoona haki haitendeki ikiwemo kukiukwa kwa taratibu, lakini haitoeleweka wanaposusia matukio makubwa ya kitaifa.

Alisema pamoja na hatua hiyo, ambayo nchi imepiga juzi na kuadhimisha kitaifa uhuru, iko haja kwa serikali kuwekeza zaidi pia jitihada zake katika kukuza demokrasia na si kwenye maendeleo ya kiuchumi pekee.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Wakili wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari alisema uwepo wa viongozi wa upinzani juzi katika maadhimisho ya Uhuru, ulitoa fursa kwao kutoa dukuduku zao kwa Rais Magufuli.

“Pale walikuwa wanatafuta fursa ta kuzungumza na kwa kweli nimefurahi kwani ujumbe umefika, kila mmoja kwa wakati wake akiwemo Mbowe (Mwenyekiti Chadema Freeman), alitumia vyema nafasi na kuelezea nini kifanyike kujenga demokrasia nchini,” alisema Profesa Safari.

Hata hivyo, alionesha kusikitishwa kwake na namna ambavyo historia ya Uhuru hailezwi vyema, kwani wapo watu walioupigania uhuru hadi kupoteza maisha, lakini hawatambuliki wala kujadiliwa.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi