loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maonesho wajasiriamali Kinondoni kuanza kesho

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema katika kuhakikisha anakuza uchumi wa viwanda, wilaya imeandaa maonesho ya wajasiriamali wa bidhaa za ngozi, yatakayofanyika Desemba 12 hadi 15, mwaka huu kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Chongolo amesema maonesho hayo yataambatana na uuzaji wa bidhaa hizo ni mkakati wa kutangaza na kuhamasisha wananchi, kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini.

Chongolo amesema lengo la maonesho hayo ni kutangaza uwezo wa wadau wa ngozi, kuelimisha jamii kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa hizo zenye ubora zinazozalishwa nchini, na kuongeza soko la ajira kwa vijana.

Amefafanua kuwa katika maonesho hayo, yatahusisha wajasiriamali kutoka wilaya ya Kinondoni pamoja na halmashauri nyingine zilizoalikwa ikiwemo Ilala, Temeke, Ubungo na Kigamboni.

Amesema kupitia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni ina wakazi zaid ya milioni 1.3.

UBALOZI wa Tanzania nchini China umetangaza kuwa kampuni ya Shandong ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi