loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Matola, Simba kimeeleweka

KLABU ya Simba imemtangaza rasmi Selemani Matola kuwa Kocha Msaidizi wa kikosi hicho huku mwenyewe akiahidi kutengeneza nidhamu ya wachezaji.

Matola anachukua nafasi ya Denis Kitambi ambaye kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza wamevunja mkataba baada ya bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Simba kufikia makubaliano naye.

“Klabu ya Simba inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Kitambi kwa mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi chake. Matola atakuwa kocha msaidizi mpya na kukaimu nafasi ya kocha mkuu wa timu ya vijana ya Simba akishirikiana na makocha wengine wa vijana,”ilisema taarifa ya Simba kwa vyombo vya habari jana.

Matola atasaidiana na kocha mpya atakayekuja kuchukua mikoba iliyoachwa na Mbelgiji, Patrick Aussems aliyetimuliwa kazi hivi karibuni. Aussems alivunjiwa mkataba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho na timu kutotimiza malengo ya kutinga makundi kenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Klabu hiyo baada ya kumalizana rasmi na Matola, iliandika ujumbe kupitia kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii: “Mtoto karudi nyumbani, tunamtangaza rasmi Matola kuwa kocha wa mabingwa wa nchi”.

Baada ya Matola kutangazwa alisema: “Najisikia furaha, unajua mimi nilikuwa mchezaji wa zamani wa Simba na Kocha wa Polisi Tanzania, nimerudi nyumbani kuitumikia Simba”.

Alisema jambo atakalofanya ni kushirikiana na benchi la ufundi kuisogeza Simba kutoka ilipo kwenda sehemu nyingine ingawa anafikiri haitakuwa kazi rahisi bali ngumu ila wamejipanga kuifanya kazi.

LEO ndio fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi