loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Miss Tanzania ang’ara Miss World

MISS Tanzania 2019, Sylivia Sebastian ametinga 20 bora kati ya warembo 120 wanaowania taji la Miss World.

Sylivia alichuana na warembo hao katika shindano dogo la kusaka membo mwenye kipaji ambapo alionesha uwezo mkubwa wa kucheza ‘Robot dance’. Muandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi alimpongeza mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram jana.

“Hongera sana Sylivia hata kwa hapo ulipofikia umetuletea heshima Tanzania kuwa katika nchi duniani zenye vipaji na sisi tupo,”alisema.

Alisema: “Hata Miss wajao wamepata pa kuanzia. Na kuendeleza ulipofikia. Umetuweka kwenye ramani. Umeweka rekodi mpya,”.

Basila alisema mafanikio ni hatua, hivyo tangu mwaka 1994 yalivyoanza mashindano hayo mwaka huu yametoa Mtanzania katika kipengele cha vipaji.

Fainali za shindano hilo zitafanyika Jumamosi ya wiki hii ambapo kiongozi huyo alimtakia mrembo huyo kila la kheri afanye vizuri zaidi.

LEO ndio fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi