loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wenger akiri kuhuzunishwa na Arsenal

ARSENE Wenger amekiri kujisikia vibaya kutokana na mweneno mbaya wa Arsenal. Mfaransa huyo alitumia miaka 22 akiwa na the Gunners, alipoanza kibarua chake tangu mwaka 1996.

Wakati akiondoka klabuni hapo mwaka 2018, Arsenal ilikuwa na mataji matatu ya Ligi Kuu ikiwemo walilolitwaa kwa kuweka rekodi ya kutopoteza mechi msimu wa mwaka 2003/04, chini yake ilitwaa makombe saba ya FA na kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa.

Masikitiko ya Wenger si kwa Arsenal pekee bali kwa soka ya England, iliyojaa mabadiliko kadhaa ya kushangaza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70 amekiri kwa namna Gunners ilivyokuwa ikicheza, ni tofauti na ilivyo sasa.

Wenger alisema: “Siku hizi, kuna klabu pengine zinawazuia kuendeleza utamaduni waliokuwa nao katika kucheza.”

“Nilipofika Arsenal, tulikuwa watu 80. Nilipoondoka walikuwa 750 na kunapokuwa na watu 750 kwenye kampuni moja kila mmoja anafikiria namna ya kujihudumia badala ya kusonga mbele.”

“Majuto yangu kwa Arsenal ni kuondoka kwenye kiwango cha utu na kukiwa na kiasi kikubwa cha uongozi, miaka 10 unaona mchezaji mzuri, unamleta, unampa suti za michezo na anakuwa sehemu ya timu.”

“Hayo yameshapita, sasa kama unamtaka mtaalamu mpya wa utimamu wa mwili, utapata maombi 300. Hivyo ndivyo ilivyo Arsenal, taratibu nilihisi klabu inaanza kuporomoka.”

LEO ndio fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi