loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC aonya wanaofanya biashara ya magendo

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata ole Sanare, amewaonya wafanyabiashara wasio waaminifu katika mkoa huo kuacha kuingiza bidhaa kwa njia ya magendo ikiwamo vipodozi vilivyozuiwa kwa matumizi ya binadamu na kuonya watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo wakati wa utoaji vyeti na zawadi kwa askari waliofanya kazi vizuri zaidi kwa mwaka 2018/2019 mkoani Morogoro. Alitoa onyo hilo baada ya Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Willbord Mutafungwa, kumueleza askari wake hawatumiki katika operesheni zinazoendeshwa na mamlaka zinazosimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali wanapokwenda kudai kodi kwa wafanyabiashara.

“Wafanyabiashara msijifiche kwa kusingizia mnadaiwa kodi kwa njia ya mtutu kwani baadhi yenu mnajihusisha na biashara za magendo ya kuficha sukari,” alisema ole Sanare. Alisema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wafanyabiashara katika mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wafanyabiashara na wawekezaji mbele ya mawaziri hazikuwa za kweli walipodai kuwa wanadaiwa kodi kwa njia ya mtutu wa bunduki.

“Nimefuatilia jambo hili kwa kina, nimepata taarifa kuwa wafanyabiashara wanaolalamika ni wale waliokuwa wameficha sukari ya magendo iliyokamatwa na polisi,” alisema.

Katika hafla hiyo iliyoambatana na maonesho ya namna ya kukabiliana na uhalifu yaliyooneshwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mkuu huyo wa mkoa pia alioneshwa sehemu ya sukari ya magendo iliyokamatwa.

Alitua halfa hiyo kumtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro asisite kuchukua hatua kwa askari ambaye atabainika kuvujisha siri za watoa taarifa za wahalifu kwani vitendo hivyo vinahatarisha amani na usalama wao.

Naye Kamanda Mutafungwa alisema katika kipindi cha mwaka 2018/2019, jumla ya askari 37 wametambuliwa na kustahili kupata pongezi maalumu kwa kazi nzuri waliyofanya mkoani humo.

LEO ndio fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi