loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mitaala mipya kufanyiwa majaribio 2022

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema mitaala mipya ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi inatarajiwa kuanza kutumika kwa majaribio ifi kapo mwaka 2022.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Simai Mohamed Said alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua mitaala mipya itaanza kutumika lini.

Said alisema mitaala hiyo imekamilika ambapo katika maandalizi yake, imewashirikisha wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika sekta ya elimu. Alisema maandalizi ya mitaala hiyo imefanyika kwa kuwashirikisha wadau ikiwemo Tanzania Bara pamoja na Kenya, Rwanda na Uganda.

Katika utafiti huo, baadhi ya marekebisho makubwa yamefanyika ikiwemo kupunguza idadi ya masomo kwa ngazi za maandalizi kutoka masomo manane hadi na kufikia masomo matano.

“Tumefanya marekebisho makubwa katika maandalizi ya mitaala kwa wanafunzi wa masomo ya msingi ikiwemo kupunguza idadi ya masomo ambayo awali yalikuwa mengi,” alisema.

Marekebisho ya mitaala hiyo yamefanyika baada ya kujitokeza kwa kasoro mbalimbali na malalamiko kutoka kwa wananchi wakiwemo wazazi. Alisema malalamiko mengi ya wazazi yamekuja kutokana na wanafunzi wengi kufanya vibaya katika mitihani yao ikiwemo ya kuingia michepuo.

“Hizo ndizo sababu zilizosababisha kufanya mapitio ya mitaala ya wanafunzi wa msingi, wazazi wanalalamika kwamba wanafunzi wao wanashindwa kupata ufaulu mzuri,” alisema.

Said alisema matarajio makubwa ya mapitio ya mitaala hiyo ni kuleta mafanikio na ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa shule za msingi kuingia michipuo na vipaji maalumu.

KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi