loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mawakili wataka kesi utekaji Mo iendelee

UPANDE wa utetezi katika kesi ya utekaji mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji maarufu ‘Mo’, inayomkabili dereva teksi, Mousa Twaleb, umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwa sababu mteja wao amekaa muda mrefu mahabusu.

Twaleb anakabiliwa na mashitaka ya utekaji wa mfanyabiashara huyo pamoja na utakatishaji fedha. Wakili wa utetezi, Mafulu Mbagwa, alitoa ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, baada ya Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, kueleza upelelezi bado haujakamilika.

Wakili Mbagwa alisema mshitakiwa huyo amekaa mahabusu muda mrefu na kwamba washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo wako nje ya nchi. Alisema kama uwezekano wa kuwakamata washitakiwa wengine haupo, basi kesi hiyo iendelee na mshtakiwa huyo kwa kuwa walishaomba nakala ya hati ya kuwakamata washitakiwa wengine lakini hawajapewa.

Hata hivyo, Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 23,mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande. Mahakama hiyo imeshatoa hati ya kuwakamata washitakiwa watano ambao ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior ambao wote ni raia wa Msumbiji na Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, mwaka jana katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini, kwa makusudi washitakiwa kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.

Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo hoteli ya Colloseum wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Pia inadaiwa Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha Sh milioni nane wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

MO alitekwa Oktoba 11, mwaka jana majira ya alfajiri maeneo ya hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi