loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima korosho wauza kwa bei juu

WAKULIMA wa korosho Mkoa wa Lindi wameuza korosho kwa bei ya juu ya Sh 2,825 na chini Sh 2,520 daraja la kwanza na pili kwa Sh 2,337.

Kaimu Mrajisi wa vyama vya msingi ushirika mkoa wa Lindi, Robert Nsunza ameyasema hayo jana. Alisema daraja la pili ilipatikana kwa chama kikuu cha ushirika cha Lindi mwambao kwenye mnada wa Jumamosi.

Alisema mnada uliofanyika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kinachohudumia wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa kiliuza tani 3,478. Alisema mnada wa Jumapili korosho ghafi tani 3,478 zote zikiwemo za daraja la kwanza bei ilikuwa Sh 2,825 na chini Sh 2,700 kwa kilo moja.

Alisema mnada wa Jumamosi bei ya juu ya korosho ilikuwa Sh 2,730 na ya chini ilikuwa Sh 2,520 kwa kilo moja daraja la kwanza. Alisema korosho daraja la pili ziliuzwa tani 150 korosho ghafi na bei ya juu ilikuwa Sh 2,337.

Aidha alisema hali ya upatikanaji wa magunia ni nzuri ambapo mpaka sasa magunia yanayohitajika 180 kwa mkoa wa Lindi. Alisema upande wa Lindi mwambao mahitaji yao magunia 60 na Runali 120.

Meneja wa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao, Nurdini Swalaa, alisema kilo 2,502,441 ziliuzwa katika mnada wa Jumamosi wiki iliyopita.

Alisema ghala la Buko bei ya juu ilikuwa Sh 2,730 na chini Sh 2,640 daraja la kwanza na daraja la pili ilikuwa Sh 2,337. Alisema ghala la Nangurukuru wilayani Kilwa bei ya juu ilikuwa Sh 2,600 na chini Sh 2,520 daraja la kwanza na pili ziliuzwa Sh 2,185 kwa kilo moja.

Alisema mahitaji ya magunia 300,000 mkoa mzima na magunia 210,000 yalishasamabazwa. Bado mahitaji magunia 90 ambayo yako bandarini. Alisema kwamba mpaka sasa tani 12,000 za korosho zilishauzwa kati ya lengo la kukusanya tani 30,000 katika msimu wa mwaka huu.

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi