loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yafurahia Brela kusajili kampuni kimtandao

SERIKALI imeridhishwa na utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kusimamia usajili wa kampuni na majina ya biashara kwa mtandao na inaandaa sheria kuboresha mazingira ya biashara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezekezaji), Angellah Kairuki alisema hayo katika mkutano wa mashauriano uliohudhuriwa na watendaji wa serikali, wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro. Alisema mkutano umebaini changamoto za uwekezaji na amependekeza namna ya kuzipatia majibu ili kuboresha mazingira ya biashara nchini.

“Hatua kubwa iliyofikiwa na Brela kupitia mfumo wao usajili wa jina la biashara na namba ya mlipa mkodi (TIN) vinapatikana sehemu moja. Jambo hili linazidi kuboresha mazingira ya biashara nchini,”alisema.

“Kuhakikisha mazingira ya biashara yanaboreshwa, Ofisi ya Waziri Mkuu inaanda muswada wa sheria mpya itakayoitwa Uwezeshaji wa Biashara itakayofanya utekelezaji wa mapendekezo yaliyopo kuwa katika blueprint”.

Alisema biashara yoyote lazima ianze na usajili wa jina au kampuni na kuwa ongezeko la viwanda Morogoro na maeneo mengine nchini ni ishara Brela imetekeleza majukumu yake katika usajili majina ya biashara na kampuni.

“Mfumo huu wa usajili kwa mtandao ni moja ya maelekezo ya serikali kwa Brela kuboresha mazingira ya biashara. Uboreshaji huu umekuwa nyenzo ya kuwavutia wawekezaji na kuifanya azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati kutekelezeka kwa vitendo,” Kairuki aliueleza mkutano huo.

Alisema wawekezaji wanatumia muda mfupi kupata usajili tofauti na nyuma ambako ililazimu mfanyabiashara kusafiri hadi Dar es Salaam kwa usajili. Aliitaka Brela na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuboresha mifumo yao wafanyabiashara wapate huduma ya majeresho ya mwaka kwa mtandao.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Roy Mhando alisema kuna ushahidi mfumo wa usajili kwa mtandao umerahisisha uanzishwaji biashara nchini kwa sababu mwananchi anaona mwenyewe gharama za usajili zimepungua.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi