loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Biteko: Anzeni kuuza 5% almasi yote Kishapu

UONGOZI wa Mgodi wa Diamond Williamson (Mwadui), unaozalisha almasi uliopo Kishapu mkoani Shinyanga, umepewa muda wa mwezi mmoja kuanza kuuza asilimia tano ya almasi yote inayozalishwa katika mgodi huo kwenye soko la ndani hususani la Kishapu, huku wazawa wakipewa fursa hiyo.

Waziri wa Madini, Doto Biteko alisema hayo juzi kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na uongozi wa mgodi wa Mwadui, alipotembelea mgodi huo na kuzungumza na wafanyabiasharaa wa madini wa soko la Kishapu.

Kisha alizungumza na wananchi wa Maganzo wilayani humo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Maganzo. “Ndugu zangu, nafurahi kuona namna mlivyokusanyika, bila shaka mna shauku kubwa ya kusikia nikisema jambo.

Kabla sijasema naomba niwaambie, Rais wetu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli amedhamiria kuona maisha ya watu yanabadilika kupitia raslimali za madini hasa wale wanaozungukwa na migodi, wakiwemo ninyi.

“Nataka nione maisha yenu yanabadilika kutokana na uwepo wa mgodi huu hapa Kishapu. Kwanza kilio chenu cha muda mrefu cha kuomba mabaki ya mchanga uliochenjuliwa (tallings) nimeagiza kuanzia tarehe 22/12/2019 mchanga ule uanze kutolewa na mkaanze kuufanyia kazi.

“Pili ifikapo Januari 2020, asilimia tano ya almasi inayozalishwa mgodini hapa wataanza kuuza kwenye soko la hapa Maganzo na watakaonunua almasi hiyo ni wazawa wanaonunua kwenye soko la Maganzo” alisema.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Diamond Williamson, Ayubu Mwenda alisema siku zote wanafanya kazi zao kwa taratibu na kwa kuzingatia sheria. Mwenda alisema hawana tatizo na uuzaji wa asilimia tano ya almasi kwenye soko la ndani, hivyo kama uongozi watatekeleza agizo la waziri na wataanza kuuza mwezi ujao. Kuhusu utoaji wa mchanga wa “makinikia” utaanza kutolewa Desemba 22, mwaka huu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Kishapu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi