loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Utapiamlo wakwamisha vita dhidi ya umaskini

TATIZO la utapiamlo linatajwa kuendelea kuathiri kasi ya kupunguza umaskini nchini. Kauli hiyo ilitolewa katika hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratias Ndejembi iliyowasilishwa kwa niaba yake na Katibu Tarafa ya Kongwa, Denis Semindu kwenye kikao kazi cha maandalizi ya awali ya mipango na Bajeti ya Afua za lishe 2020/2021.

Semindu alisema, lishe duni si tu huathiri tu maendeleo ya mtoto katika ukuaji, bali humuathiri kimwili, kiakili tangu kipindi cha ujauzito na kuathiri mchango wake wa maendeleo kipindi chote cha uhai wake.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Taifa wa Hali ya Lishe 2018/2019 kwa watoto chini ya miaka mitano, Dodoma ina asilimia 37.2 ya utapiamlo. Pia kwa takwimu za afya wilayani Kongwa asilimia 24 ya watoto waliohudhuria kliniki kuanzia Januari hadi Desemba 2018 wameonekana wana uzito pungufu na watoto 235 wana utapiamlo.

Naye Mtaalamu wa Masuala ya Lishe, Eloy Sigalla akitoa mada alisema lishe yenye kuzingatia makundi yote ya chakula ina umuhimu mkubwa sana katika siku 1000 za makuzi ya ubongo kwa mtoto yaani siku 270 za mimba, siku 365 mwaka wa kwanza 365 za mwaka wa pili.

Sigalla aliainisha baadhi ya sababu za utapiamlo kuwa ni pamoja na ulaji duni, ukosefu wa chakula, ukosefu wa huduma za afya, mila na desturi ambapo kuna baadhi ya makabila hukataza wajawazito ulaji wa baadhi ya vyakula kwa hofu ya mtoto kuzaliwa wanene na mgawanyo duni wa vyakula na sababu zao zingine za kimila.

Ofisa Lishe wilayani Kongwa, Maria Haule akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli za lishe alisema pamoja na changamoto za upungufu wa wataalamu wa hali ya lishe, changamoto kubwa katika utekelezaji wa shughuli za lishe ni upatikanaji wa fedha hii inaleta ugumu kufikia malengo yaliwekwa na kamati hiyo katika kupambana na utapiamlo.

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesisitiza ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Kongwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi