loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Elimu ya gerezani kumnufaisha

BAADHI ya wafungwa wanufaika wa msamaha wa Rais John Magufuli mkoani Morogoro akiwamo Josam Gabriel aliyehukumiwa miezi sita na kifungo chake kilipaswa kumalizika Januari 11, 2020, amemshukuru Mungu pamoja na Rais kwa msamaha huo, na akiwa anatumikia kifungo alipatiwa ujuzi ukiwamo wa kupika vyakula na ujenzi.

Wafungwa 365 waliokuwa wakitumikia vifungo vya miaka tofauti katika magereza zaidi ya 12 mkoani Morogoro wameachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli wakiwemo wanawake watatu.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Sylvester Mrema alisema hayo juzi wakati akitangaza majina ya waliopatiwa msamaha mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ya Wilaya ya Morogoro. Mrema aliyataja Magereza waliotoka wafungwa walioachiwa huru kwa msamaha huo na idadi yao kwenye mabano ni Kiberege (63), Mtego wa Simba (31), Mahenge (9), Kilosa (23), Wami Vijana (10), Idete (57), Kihonda (49), Gereza la Mahabusu (36), Mbigiri (36), Wami Kuu (26) Mkono wa Mara (11) na Gereza la Wanawake Kingolwira (3).

Akizungumzia msamaha huo, Gabriel alisema akiwa mpishi mzuri pia aliongeza ujuzi wa ujenzi na baada ya msamaha huo akiwa uraiani atatumia ujuzi huo kwa manufaa yake kujipatia kipato na jamii inayomzunguka.

“Nitakuwa mtu mwema na mwenye maadili kama dini ya wazazi wangu inayoelekeza na kanisa pia,” alisema.

Mwingine Steven Chambo ambaye alifungwa miaka mitatu kwa kosa la mauaji bila kukusudia, pia alimshukuru Rais kwa kumpatia msamaha huo kwani alipaswa kutoka gerezani Aprili 2020 na kwamba alishangaa kuitwa jina la kusamehewa kuendelea na kifungo chake jela.

Kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi