loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malinzi ahukumiwa, akwepa kutupwa jela

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Sh 500,000 aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa.

Vigogo hao wa TFF walihukumiwa kifungo hicho au kulipa faini baada ya kutiwa hatiani kwa mashitaka ya kughushi muhtasari wa Kikao cha Kamati Utendaji ya shirikisho hilo. Hata hivyo, pamoja na washitakiwa hao kukubali kulipa faini, walilazimika kuendelea kukaa mahabusu hadi leo watakapolipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Pia mahakama hiyo iliwaachia Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani wa shirikisho hilo, Flora Rauya kwa sababu upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha pasi na shaka mashitaka dhidi yao. Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa 5, aliyesikiliza kesi hiyo, Hakimu Maira Kasonde alisema upande wa mashitaka ulileta mashahidi 15 kuthibitisha mashitaka hayo.

Alisema upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha mashitaka mawili ya kughushi muhtasari wa Kikao cha Kamati tendaji ya TFF linalowakabili Malinzi na Mwesigwa pamoja na la kutoa nyaraka ya uongo linalomkabili Mwesigwa peke yake. Alisema katika mashitaka hayo, kila mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miaka miwili jela ambapo kwa upande wa Mwesigwa, atatakiwa kulipa faini ya Sh 1,000,000.

Hakimu Kasonde alisema washitakiwa wote walikuwa wanakabiliwa na mashitaka 30 na baadaye mahakama iliwaona hawana kesi ya kujibu katika mashitaka 10 ambayo ni ya matumizi mabaya ya ofisi, kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Alisema katika mashitaka ya kujipatia fedha ambayo yalimkabili Malinzi, upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha mashitaka hayo kwa sababu fedha alizozipata Malinzi kutoka TFF alikuwa akijilipa deni alilokuwa akidai shirikisho hilo kama ilivyothibitishwa na maofisa wanne wa shirikisho hilo. Pia alisema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo kwa kutoleta ripoti ya ukaguzi ya kuonesha fedha zilizopokelewa ni halali au la.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha yaliyowakabili Malinzi, Mwesigwa na Nsiande, Hakimu Kasonde alisema mashitaka hayo hayajathibitishwa kwa sababu fedha anazodaiwa kupokea Malinzi ambazo ni Dola za Marekani 173,335 na Sh 39,100,000 ni marejesho ya mkopo aliokopesha

JUMLA ya mapambano 10 ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi