loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wengi wachangamkia vifurushi vipya vya NHIF

IKIWA ni takribani wiki mbili tangu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), itangaze vifurushi vipya, tayari wananchi 1,848 wameshajiunga na huduma hizo.

Pia, NHIF inatarajia kuanza bidhaa mpya wa Machinga Afya, ambayo itawahusisha wajasiliamali huku mfuko huo ukilipa jumla ya Sh trilioni 1.283 kwa vituo vyote vinavyowahudumia wanachama wake. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alipozungumzia mafanikio ya NHIF katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Rais John Magufuli wakati ziara ya timu ya maofisa habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na taasisi zake.

Konga alisema katika kuongeza wigo wa kuwafikia wananchama, NHIF imeweka utaratibu rahisi unaomwezesha kila Mtanzania kujiunga na huduma za bima ya afya kulingana na mahitaji yake kwa kuanzisha vifurushi vipya vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya ambapo mpaka sasa wanachama 1,848 wameshajiunga.

“Vifurushi hivi vimezingatia hali halisi ya wananchi na vinamwezesha kujipimia kulingana na uwezo wa kuchangia, mahitaji ya huduma, umri na idadi ya wanufaika na tangu tuzindue Novemba 28 na usajili kuanza mikoa yote tayri wanachama 1,848 wameshajiunga huku lengo likiwa ni kuwandikisha wanachama wapya milioni 1 kwa mwaka,” alisema.

Aidha, Konga pia wanatarajia kuanzisha huduma nyingine kwa wajasiliamali kupitia Machinga Afya na kwa sasa wako katika hatua ya kuwasajili wajasilimali 8,000 wa soko la Kariakoo.

“Wanachama wetu kwa asilimia 99 ni watumishi wa umma, na pia tunawatumishi wa sekta binafasi, lakini tulioana tuje na bidhaa mbalimbali ili kuwafikia asilimia 80 ya watanzania ambao wako katika sekta isiyorasimi.

“Ili kuwafikia hao tumeanzisha bidhaa mbali nah ii ya vifurushi vyipya, pia kuna ya wakulima kupitia Ushirika Afya iliyoanza mwaka jana na tayari tumeshawafikia wanachama 2,000, tuna Toto Afya Kadi kwa watoto chini ya miaka 18 ambapo mpaka sasa tunawanachama 100,000 na pia tunataka tuwafikie waendesha bodaboda kupitia Bodaboda Afya na Umoja afya kwa ajili ya makundi mbalimbali wakiwamo mama lishe,” alieleza.

Kwa sasa NHIF wanachama 966,792 sawa na wanufaika 4,025,693, ikilinganishwa na wanufaika 3,237,434 wa mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 20. Akizungumza mchango wa NHIF katika uimarishaji wa huduma za matibabu, Konga alisema kwa miaka minne wametoa jumla ya Sh bilioni 13.7 zilizotumika kukarabati miundombinu na ununuzi wa vifaa vya matibabu kama MRI, CT-Scan na uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuzalisha maji na gesi inayotumika kwa wagonjwa. Baadhi ya hospitali zilizonufaika na uwekezaji huu ni Muhimbili, Bugando, ORCI, KCMC, Rufaa Mbeya na MOI.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi