loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi waomba sheria ndogo kuwaondolea ‘utata’

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Manchali wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamependekeza kuwapo kwa sheria ndogondogo zitakazowatengenezea mazingira salama ya kusoma bila kuwa na adhabu za kuudhi kama kuchimba visiki.

Walisema hayo wakati wakitoa mapendekezo ya kutengeneza sheria ndogondogo kuanzia shuleni, nyumbani, kwenye nyumba za ibada na kwenye serikali za vijiji, vitongoji. Walikuwa wakizungumza jana kwenye mwendelezo wa Mradi wa Sauti Yangu unaotekelezwa na Shirika la Woman Wake Up (Wowap), unaofadhiliwa na Shirika la Child Fund Korea kupitia Jukwaa la Haki za Watoto.

Wakiwasilisha mapendekezo kwa niaba ya wenzao, mwanafunzi Anitha Mazengo wa kidato cha tatu alisema wanataka sheria ndogo kuwazuia pia walimu kuwatuma wanafunzi wakati wa vipindi vya darasani na walimu waandike wenyewe ubaoni na kuacha tabia ya kuwaachia kazi kuachia wanafunzi ambao baadae hukosa muda wa kujisomea.

Pia walitaka walimu kupunguza adhabu kali kwa wanafunzi ikiwemo kuchimba visiki na watoto wasikilizwe kabla ya kupewa adhabu.

“Tunataka kupunguziwa adhabu kali kama kuchimba visiki kwani mwanafunzi anapopata wastani chini ya 50 hupewa adhabu hiyo, itafutwe adhabu mbadala kama kufanya usafi.

“Tunataka sheria ya kusitishwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa walimu kuwataka kimapenzi wanafunzi na hata wanafunzi kutongoza wanafunzi wenzao.”

Wanafunzi hao walitaka muda wa kuruhusiwa kutoka shuleni uongezwe kutoka saa 8:30 mchana hadi saa 10 ili waweze kupata muda wa kujisomea. Katika sheria zinazohusu serikali za vijiji walitaka wanafunzi kushirikishwa kwenye vikao mbalimbali vya maendeleo, pia viongozi kutenda haki kwa usawa kwani kiongozi anapopewa rushwa kesi zinaishia hewani.

Kwenye maoni juu ya nyumba za ibada walipendekeza kupunguza muda wa wanafunzi kuimba kwaya au kwenda kwenye makongamano ya kidini ili wanafunzi wapate muda zaidi muda wa masomo na ikiwezekana waruhusiwe wakati wa likizo tu. Pia vipindi vya dini shuleni viongozwe na mapadiri, wachungaji au mashehe na si wanafunzi.

Akitoa maoni ya mapendekezo ya sheria ndogo ndogo zinazotakiwa kuwepo nyumbani kwenye familia mwanafunzi, Amon Sangaya wa kidato cha tatu alitaka wazazi kushirikisha watoto kwenye kuuza mali za familia, ikiwemo mifugo na mashamba.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Chamwino

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi