loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Katibu Mkuu CCK mbaroni tuhuma za rushwa mil. 50/-

KATIBU Mkuu wa Chama cha Siasa Cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (pichani) anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh milioni 50, akijifanya ni mtumishi wa Takukuru.

Aidha, katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, Takukuru Ilala walipokea malalamiko yanayohusu rushwa 180, yasiyohusu rushwa 62, majalada yaliyofunguliwa kutokana na malalamiko mapya 42.

Mkuu wa Takukuru Ilala, Christopher Myava aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Desemba 10, mwaka huu, jioni katika ofisi ya Bharya Engineering and Contracting Company Limited (BECCO) alipokea fedha za mtego wa rushwa ya Sh milioni moja. Alisema mtuhumiwa huyo alijifanya mtumishi wa Takukuru na kumuahidi Mkurugenzi wa BECCO, Manraj Bharya ampe rushwa ya Sh milioni 50 ili amsaidie katika tuhuma alizokuwa anakabiliana nazo za Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL).

“Tulimkamata mtuhumiwa huyu siku hiyo baada ya kuwekewa mtego wa shilingi milioni moja alizozipokea akijifanya atasaidia kumaliza tatizo hilo,” alisema.

Alisema baada ya kupata taarifa ndiyo aliwekewa mtego na kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa akiwa anapokea fedha hizo kutoka kwa mkurugenzi wa Becco. Myava alisema uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi