loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Safisha mafisadi CCM yapaisha pato

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amebainisha kuwa baada ya kuwaondoa mafi sadi waliokuwa wanatafuna mali za chama hicho, sasa thamani ya mali za chama hicho imepanda huku mapato yake yakifi kia kiasi cha Sh bilioni 59.8 kwa mwaka.

Awali, alivyochukua nafasi ya Uenyekiti ndani ya chama hicho, kilikuwa kiingiza mapato ya Sh bilioni 46.1 kwa mwaka, huku mali zake nyingi zikiwa chini ya watu wachache hali iliyokifanya kuwa hoi kiuchumi na kuwa ombaomba licha ya kuwa na mali nyingi. Dk Magufuli aliyasema hayo jijini Mwanza jana wakati akifungua semina ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, iliyotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya televisheni.

“Nilipopewa ridhaa ya kuongoza chama, nilitambua haja ya kufanya mageuzi makubwa ndani ya chama, kimuundo, kiutendaji na kiuchumi lengo ni kuondoa urasimu na kuongeza ufanisi na kukijenga chama kiuchumi,” alieleza Rais Magufuli.

Alisema mageuzi hayo, yalikuwa hayaepukiki ili kujenga imani ya chama kwa wanachama lakini pia kujenga serikali imara hali ambayo pia itazaa taifa imara. Alisema kwa upande wake, hali ya chama hicho kiuchumi na hata kimuundo haikuwa inafurahisha jambo lililomuia vigumu kuzungumzia mageuzi makubwa ndani ya serikali ilihali chama tawala kiko hoi.

Alitaja mageuzi aliyoyafanya kwenye chama hicho kuwa ni pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe NEC kutoka 342 hadi 168 na kuwaondoa makatibu wa mikoa katika orodha ya wajumbe wa NEC kwa sababu ni watendaji. Pia alitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuondoa kada ya Katibu Msaidizi na mhasibu wa wilaya na mkoa na majukumu yao kutekelezwa na katibu mmoja wa wilaya na mkoa.

Aidha, alisema aliamua kuunganisha utumishi wa chama na jumuiya ili uwe chini ya Sekretarieti ya NEC na kufuta nafasi ya Katibu wa NEC wa Mkoa hadi Tawi. Dk Magufuli alifafanua kuwa pamoja na wingi wa mali za CCM mapato ya chama hicho yalikuwa kidogo sana kiasi cha chama kushindwa kujiendesha. “Mali nyingi ziliwanufaisha wachache na baadhi ya viongozi walijimilikisha mali hizo.

Chama kikabaki kuwa ombaomba na kutegemea fedha za matajiri wachache waliojiita wafadhili wa chama,” alieleza.

Alisema matajiri hao wachache ndio walikuwa na maamuzi makubwa ndani ya chama na hakukuwa na mtu aliyefurukuta. Tukasema haiwezekani kamwe uozo huu uendelee chini ya uenyekiti wangu na uongozi wenu, tukachukua hatua,” alisema.

Alifafanua kuwa hiyo ndio sababu ya kuunda tume ya uhakiki wa mali za CCM chini ya Dk Bashiru Ali (sasa Katibu Mkuu wa CCM Taifa). “Tume hiyo ilifanya kazi kwa weledi na kubaini kuwa kwa miaka mingi CCM ilikuwa ni shamba la bibi, kila mtu alikuwa akitafuna mali za chama mahali alipo,” alisema.

“Tukaanza kazi ya kurejesha mali za chama ikiwemo vyombo vya habari kama Chaneli 10, ambayo pamoja na kuwa mali ya CCM lakini haikuwa chini ya CCM, tukarejesha majengo, vituo vya mafuta, vitalu,” alisisitiza.

Aidha, alisema katika mageuzi hayo pia walipitia upya mikataba ya uwekezaji, ikiwemo Vodacom, jengo la Umoja wa Vijana Dar es Salaam na kuanzisha mfumo wa eletroniki wa usimamizi wa mali na rasilimali za chama hicho. Alisema jitihada hizo za udhibiti wa mapato ya chama kupitia makao makuu, zilisaidia kuongeza mapato ya CCM kutoka Sh bilioni 46.1 mwaka 2015/16 hadi Sh bilioni 59.8 mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 30.

Alisema pia baada ya kuthaminisha upya mali za chama, thamani yake imeongezeka kutoka Sh bilioni 41.033 mwaka 2016/17 hadi Sh bilioni 974.66 sawa na ongezeko la asilimia 2,275.2.

“Nimearifiwa zoezi la tathmini limefanyika katika mikoa 13 tu nina uhakika mikoa mingine nayo itafanyika tathmini na mali za chama zitakuwa ni mabilioni kwa mabilioni,” alisisitiza.

Alisema endapo wataendelea na jitihada hizo, CCM itaweza kujitegemea kwa asilimia 100 na kuachana na kutegemea fedha za wafadhili. Pia maslahi ya watumishi wa chama yataongezeka.

Akizungumzia mafanikio ya kiuanachama ndani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka minne alieleza kuwa chama hicho kimepokea wanachama mbalimbali kutoka upinzani na kusababisha kuongezeka kwa ruzuku kutoka Sh bilioni mwaka 12.4 2015/2016 hadi Sh bilioni 13.5 kwa mwaka hivi sasa. Alisema mwelekeo wa sera za CCM kwa kipindi cha miaka 10, kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 ilijielekeza kujenga uchumi wa kisasa na kuwawezesha wananchi.

“Ilani ya uchaguzi 2015/20 iliandaliwa kuelekea mwelekeo huo. Hata hivyo, alikiri kuwa serikali haikutumia ilani kama Msahafu au Biblia kwani pamoja na kutumia ilani hiyo katika kutekeleza mambo mengi lakini serikali haikujizuia kufanya jitihada nyingine zenye maslahi kwa taifa.

“Tuliona kuna umuhimu wa kuangalia mahitaji halisi ya watanzania na kuchukua hatua muafaka na kukubaliana kuwa kuna baadhi ya hatua zinapaswa kuchukuliwa hata kama hazipo kwenye ilani,” alisisitiza.

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi