loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aliyesamehewa na JPM akamatwa kwa wizi wa ng’ombe

MKAZI wa Mikoroshini Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Mustafa Malimi (23) ambaye ni mmoja ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais John Magufuli Desemba 9 mwaka huu, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba ng’ombe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa jana, ng’ombe aliyeibwa alikutwa amechinjwa na mtuhumiwa huyo. Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea Desemba 11 mwaka huu saa 4:00 asubuhi huko Nero Magorofani wilaya ya Chalinze.

“Mtuhumiwa aliiba ng’ombe mwenye thamani ya Sh milioni 1.2 mali ya Otaigo Elisha (30) mkazi wa Pera Chalinze,” alisema. Dereva Baraka Njoka (37) mkazi wa Ubungo Kibo anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mafuta ya kula madumu 860 ambayo hayakulipiwa ushuru wa forodha. Kamanda Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea Desemba 11 mwaka huu saa 8:20 usiku Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 582 AWB likiwa na mafuta hayo. “Mafuta hayo ya kampuni ya Mico na Oki yalikuwa hayana kibali chochote wala hayakulipiwa ushuru wa serikali,” alisema.

Aidha alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi