loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Daktari aonya kuhusu unywaji maji kidogo

WATU wanaokunywa kiwango kidogo cha maji ikilinganishwa na chumvi inayotengenezwa mwilini wako katika hatari ya kupata matatizo ya mawe kwenye fi go na mfumo wa mkojo.

Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa Mfumo wa mkojo na upandikizaji wa figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dk Remigius Rugakingira. Dk Rugakingira aliwaambia maofisa habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zake katika Kanda ya Kati kuwa matatizo ya mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo ni unywaji wa kiwango kidogo cha maji ikilinganishwa na kiwango cha chumvi ambacho mwili unatengeneza.

“Kama unakunywa maji kidogo kulinganisha na aina ya chumvi inayotengenezwa mwilini una hatari ya kupata mawe, pia kuwa na bakteria wengi katika mfumo wa mkojo unaweza kutengeneza mawe,” alisema.

Dk Rugakingira alisema awali hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wastani wa wagonjwa watano kwa mwezi, lakini hivi sasa ni wastani ni wagonjwa 32 kwa mwezi.

“Asili ya mawe ambayo tunayaona ni magumu na tuna historia hapa tulitoa jiwe lenye sentimita 4.5 ambalo tumetoa kwenye kibofu, sentimita 2.6 ambalo limetolewa kwenye figo na kuwa na aina hii ya mawe yanaleta shida kwenye njia ya mkojo kama vile kutotoka mkojo wa kutosha,” alisema.

Aidha, Dk Rugakingira alisema katika kuboresha utoaji wa huduma, hospitali hiyo inatarajia kufunga mashine mpya ambayo itawasaidia kuyeyusha mawe kwa njia ya kisasa zaidi ambayo itagharimu Sh bilioni sita.

“Uwekezaji wa mashine hii ni mkubwa na wa kisasa ni sawa na Ujerumani na nchi zingine, itatumia mionzi kwa hiyo itakuwa unatumia kamera, unaenda kwenye eneo la jiwe na kulivunja, njia nyingine ya pili ni kutumia mfumo wa kufungua, hivyo itatufanya tuwe na uwanja mpana wa kutoa matibabu badala ya kufanya upasuaji wa kuchana,”alisema.

Kutokana na ubora wa huduma ambazo wamekuwa wakizitoa wameweza kupata wagonjwa kutoka nje ya Tanzania na kuzitaja nchi hizo kuwa ni Comoro, Saudi Arabia, Ghana na Uganda ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi