loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndege iliyokamatwa Canada kupokewa leo

RAIS John Magufuli anatarajia kuongoza maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza leo, kupokea ndege aina ya Bombadier Q 400 kutoka Canada. Ndege hiyo ni ya pili kukamatwa na mzungu mkulima wa Afrika Kusini, Hermanus Stern kwa muda wa wiki tatu sasa.

Nyingine iliwahi kukamatwa Afrika Kusini hivi karibuni. Hayo yamesemwa jana jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa ndege hiyo hapa nchini kupitia Mwanza. Pia, alizungumzia ujio wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuipokea ndege hiyo.

“Niwaombe wananchi wa mkoa wetu na mikoa jirani, wajitokeze kwa wingi kuipokea ndege yao baada ya wanasheria wazalendo kuipigania ndege hiyo katika mahakama za nchini Canada hivi karibuni na kufanikiwa,” alisema.

Rais Magufuli alitangaza ujio wa ndege hiyo, alipokuwa akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi jijini Mwanza wiki hii. Alisema ndege hiyo imeachiwa kutoka Canada na mapokezi yake yangefanyika jijini Mwanza. Moja ya mambo makubwa ambayo Serikali ya Rais Dk Magufuli imeyafanya baada ya kuingia madarakani mwaka 2015 ni kuifufua Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), ambayo hali yake ilikuwa mbaya.

Ilichokifanya serikali ni kununua ndege mpya na za kisasa ambazo imeikodisha ATCL. Kutokana na juhudi hizo za serikali, kwa sasa ATCL ina jumla ya ndege mpya nane, ambazo ni Boeing 787-8 Dreamliner mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 262 kila moja na Airbus A220-300 mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.

Ndege zingine ambazo zimeshawasili nchini na zinaendelea kutoa huduma ni Bombardier Dash 8 Q400 tatu, zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, na ndege nyingine mpya ni Bombardier Dash 8 Q400 ndiyo itakayowasili leo.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi