loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC Makonda akusanya mil 120/- kwa ajili ya watoto wa moyo

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza kampeni yake ya kutibu watoto zaidi ya 500 kwa mwaka 2020 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kukusanya Sh milioni 120 kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za umma na makampuni binafsi zitakazowezesha matibabu ya watoto 60 kwa mwezi Januari na Februari mwaka 2020.

Hiyo ni baada ya kampeni ya awali ya kusaidia matibabu ya watoto 60 kwa mwaka 2019 kumalizika kwa mafaniko ambapo watoto hao 60 walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwashukuru wadau waliojitolea kuchanga pesa hizo Mkuu wa Mkoa alisema kuwa baada ya kukamilisha ahadi ya kutibu watoto 60 akaona kuna umuhimu wa kuongeza namba ya watoto watakaotibiwa mwaka 2020 lakini akagundua gharama za kukamilisha matibabu hayo ni kubwa na alihitaji msaada hali iliyomfanya akaamua kuunda Kamati iliyoongozwa na Mwenyekiti Dk Charles Kimei.

“Hakuna kitu kinauma kama mzazi kuona anashindwa kumuondolea maumivu mtoto wake kwa kukosa pesa za matibabu, hiyo ndiyo sababu kubwa inanifanya nitafute msaada wa matibabu kwa watoto hawa lakini kutokana na namba na gharama kuwa kubwa niliyoambiwa niliamua kuunda timu ili inisaidie kutafuta hiyo pesa ndipo nilipoamua kumkimbiliza mzee wangu mzee Kimei anisaidie kufanya hii kazi, hatimaye leo mnaona tumefanikiwa kupata kiasi cha kuanza matibabu kwa mwezi Januari na Februari,” alisema.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi