loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Ditram Nchimbi atua Yanga

Uongozi wa klabu ya Azam FC umethibitisha kuwa wamemalizana na klabu Yanga kuhusu usajili wa mshambuliaji Ditram Nchimbi aliyekuwa kwa mkopo Polisi Tanzania.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Iddi amesema Yanga iliwaandikia barua kumuhitaji mshambuliaji huyo ambaye yuko kwenye kiwango bora akiwa na timu ya taifa ya Tanzania bara Kill stars nchini Uganda.

Makubaliano kati ya klabu hizo yamefikiwa baada ya mchezaji mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kuhamia Yanga.

Azam FC waliitaka Yanga walipe gharama za mchezaji kwa muda uliobaki wa miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika.

Kwa mujibu wa Idd, Azam FC walikuwa na nia ya kuongeza mkataba na Nchimbi lakini baada ya mchezaji mwenyewe kuonyesha nia ya kuondoka wameamua kumuachia.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

2 Comments

 • avatar
  FRED MULLAH
  18/12/2019

  NCHIMBI KARIBU JANGWANI UPIGE KAZI

 • avatar
  marko rabshake
  19/12/2019

  club yayanga FC yapaswa kuwamakini juuya usajili wawa chezajiwao kulingana na sifaza club na mchezaji.by marko haule from dodoma sitjohn

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi