loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pogba kuendelea kukaa nje Man United

MCHEZAJI wa Manchester United, Paul Pogba atachelewa kurudi uwanjani baada ya kukosa mazoezi ya siku mbili kwa sababu ya ugonjwa.

Kiungo huyo wa Ufaransa alitarajiwa kurudi kwenye mazoezi wiki hii baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu ambalo lilimuweka nje tangu Septemba. Pogba alihudhuria harusi ya kaka yake huko Ufaransa, Ijumaa iliyopita, lakini alihitaji kufanyiwa vipimo na daktari wa United siku ya Jumamosi lakini alizidiwa siku ya Jumapili.

“Ameshindwa kuja kwa sababu anaumwa, Hajafika mazoezini kwa siku mbili kwa sababu anaumwa sana,” alisema bosi wa United, Ole Gunnar Solskjaer.

Pogba amecheza mechi sita tu msimu huu, anahitaji upasuaji ili kurekebisha shida ya kifundo. Solskjaer, ambaye anakabiliwa na mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Carabao nyumbani Jumatano, alikataa maneno ya mashabiki wanaodai hawezi kushinda bila Pogba. Alisema walimkosa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton na walitoka sare ya 1-1 Jumapili iliyopita.

“Mchezo kama wa Everton, kwa mfano, tulikosa nini. Kutengeneza pasi au ubunifu? Ana ubora wake, sio kila viungo duniani anao, kwa hivyo itakuwa vizuri kumrudisha,” alisema Solskjaer.

Solskjaer anatarajia kufanya mabadiliko ya kikosi kitakachoanza katika ziara yake ya kwanza ya Colchester ya kutembelea Old Trafford. Hiyo ina maana kuwa mshambuliaji kinda Mason Greenwood ambaye alifunga bao lake la saba msimu huu dhidi ya Everton. Ni vigumu kwa sasa kumweka nje Mason, yupo akilini mwangu, “alisema Solskjaer kudai hata yeye alikuwa mshambuliaji tegemeo wa klabu yake kati ya mwaka wa 1996 na 2007.

“Nakumbuka nilipokuja klabuni na kufunga mabao kadhaa, nilihisi ningeweza kufanya vizuri zaidi, Meneja alisema ni ngumu kuwaweka nje wachezaji ambao wanafunga mabao. Ni sawa na Mason,” aliongeza Solskjaer.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi