loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waandishi wasitumiwe na wanasiasa

MSEMAJI Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas amewataka waandishi wa habari nchini kutotumia wanasiasa kutafsiri taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa lengo la kupotosha maana kwa umma.

Dk Abbas alisema hayo juzi mjini Dodoma wakati akitoa mada ya Wajibu wa Wanahabari kuandika ripoti za CAG katika semina iliyojumuisha waandishi wa habari na asasi za kiraia (NGOs).

Alitoa mfano waandishi walivyopotosha ripoti ya CAG ya mwaka ulioishia Juni, 2017 wakidai kuwepo upotevu wa Sh trilioni 1.5 na Sh trilioni 2.4 mwaka ulioishia Juni, 2018 wakikariri tafsiri za wanasiasa katika uchambuzi ambao si sahihi.

Aliwataka wanapoandika ripoti za CAG wazitoe kama zilivyoainishwa na kama ni uchambuzi, basi uwe wao na si kuwakariri wanasiasa.

Alisema waandishi wengi wanakosa uelewa wa kutosha katika masuala ya fedha na ukaguzi hivyo kushindwa kuchambua taarifa za ukaguzi.

Tumeguswa na maelekezo ya Dk Abbas na kuungana naye kuwataka waandishi nchini kote kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi kwa lengo la kujenga imani ya wananchi kwa serikali yao, kuimarisha demokrasia na uhuru.

Si sahihi hata kidogo kwa waandishi wa habari nchini kutumia vibaya uhuru wa vyombo vya habari kupotosha umma kuhusu taarifa rasmi za fedha za serikali yao na idara zake wakiegemea tafsiri potofu za wanasiasa wanaoipinga serikali.

Tunakubaliana na Dk Abbas waandishi habari wenye tabia hiyo au vyombo vyao waadhibiwe kwa kukiuka maadili na kanuni za uandishi wa habari ili iwe fundisho kwa watu wengine wote.

Kwa wanasiasa pia tunasema iko haja kwa wenye tabia hiyo kuacha kutumia propaganda chafu kupotosha umma kwa lengo la kubeza kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM.

Kama kuna upungufu wowote, ni vyema wale wanaoamini upungufu huo unastahili kusemwa wazingatia miiko na maadili ya utoaji habari na pia kukosoa serikali kwa mujibu wa taratibu ikiwemo kusema bungeni au kuita waandishi.

Wakati huu tunapoelekea mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka mpya, 2020, tunaomba kila mwandishi wa habari kujikumbusha kanuni na maadili ya kazi ili kulinda heshima ya taaluma.

Kinyume chake, tutawachukulia wao binafsi na vyombo vya habari wanakofanyia kazi kama wanaolenga kuchochea vurugu nchini ama kwa kutumiwa na watu wa nje wanaoitakia nchi yetu mabaya au maslahi yao binafsi kukidhi haja zao.

Kama hivyo ndivyo, tuwakumbushe kwamba basi wakae wakijua kuwa serikali iko macho, imara na haitakaa kimya na kuwafumbia macho.

WATANZANIA kupitia vyama mbalimbali vya siasa, wapo katika mchakato wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi