loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lissu hatarini kukamatwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imesema itafuta fungu la dhamana, alilosaini mdhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Ibrahim Ahmed endapo hatamleta mshitakiwa huyo mahakamani.

Awali, Mdhamini wa Lissu, Ahmed aliieleza mahakama kuwa aliwasiliana na Lissu kama mahakama ilivyomuelekeza kwamba afike siku ya kesi (jana).

Alidai alichojibiwa na Lissu (pichani) ni kwamba anahitaji kuja nchini, lakini bado ana shaka na kwamba anaendelea kumhimiza kufika mahakamani kusikiliza kesi yake. Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai kutokana na maelezo ya mdhamini huyo, hawaelewi kama mshitakiwa bado mgonjwa au ameshapona na kwamba wanao mashahidi, lakini hawawezi kuwaleta kutokana na mshitakiwa huyo kutofika mahakamani.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema “Bado naendelea kusisitiza namtaka mshitakiwa hapa mahakamani, kwa sababu shauri hili limekaa muda mrefu linashindwa kuendelea. Hivyo, mlete mshitakiwa kabla fungu lako la dhamana halijafyekwa.” Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 20, 2020.

Alisisitiza Lissu kufika mahakamani na kwamba dhamana kwa washitakiwa wengine inaendelea. Mbali na Lissu na Simon Mkina, washitakiwa wengine ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob. Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano, ikiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washitakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar’. Katika mashitaka ya pili, wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshitakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi. Inadaiwa mshitakiwa huyo, pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Mbali na mashitaka hayo, washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar, wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi