loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Manchester City, United vita inaanza upya

MICHUANO ya Kombe la Carabao yamefi kia patamu baada ya timu za Manchester City na Manchester United kukutana kwenye nusu fainali ya michuano hiyo huku Aston Vila ikiwa na kibarua cha kuivaa Leicester City, michezo itakayopigwa wiki tatu zijazo.

Manchester United ilifika hatua hiyo baada ya juzi kushinda mabao 3-0 dhidi ya Colchester United, huku Manchester City ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Oxford United, Aston Villa iliifunga Liverpool mabao 5-0, wakati Leicester City iliifunga Everton kwa penalti 4-2, baada ya mchezo kuisha sare ya 2-2.

Mchezo wa kwanza utakaopigwa Januari 6, Manchester City italazimika kusafiri hadi katika Uwanja wa Old Trafford kusaka tiketi ya kucheza fainali ya tatu mfululizo, wakati kwa upande wa kocha wake Ole Gunnar Solskier atakuwa na shauku ya kufika fainali yake ya kwanza tangu kufukuzwa kwa Jose Mourinho.

Leicester City itakuwa nyumbani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Aston Villa, kusaka nafasi ya kucheza fainali yake ya kwanza tangu mwaka 2000 ilipochukuwa ubingwa huo kwa kuifunga Tranmere Rovers mabao 2-1.

Kuelekea mchezo wa mahasimu wawili wa jiji la Manchester, Kocha ya United, Solskier alisema anawaheshimu wapinzani wake hasa kutokana na ubora walionao na kwamba licha ya ubora wao anajiamini hasa baada ya kufika hatua hiyo.

Alisema wanahitaji kufikiria zaidi namna ya kushinda mchezo huo na kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na kuongeza kuwa ana uhakika lolote linaweza kutokea hasa baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

“Tumewaonesha kuwa hata sisi tunaweza kusababisha matatizo kwenye sehemu yao ya ulinzi kwa hiyo tupo tayari kwa mchezo, kwa maoni yangu ni timu bora England lakini tutapambana nao,”alisema Solskier

. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote lakini taarifa njema kwao huenda beki John Stones na mshambuliaji Sergio Aguero wakarejea na kuwa sehemu ya mchezo huo.

Alisema baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Oxford United ni imani yake kuwa baada ya wachezaji hao kurejea na kuongeza nguvu watakuwa na matumaini mazuri ya kufika fainali kwa mara nyingine.

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania rasmi ametolewa kwa mkopo ...

foto
Mwandishi: MANCHETER, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi