loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Yanga yashusha kifaa kingine

KLABU ya Yanga imeendelea na usajili, baada ya jana kushusha mshambuliaji mwingine kutoka Ivory Coast, Yikpe Gnamien aliyekuwa akicheza Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema mchezaji huyo walikuwa wamemalizana naye kwa maongezi na alikuja kwa ajili ya vipimo na kusaini mkataba.

“Tulikuwa tumeshamalizana naye amekuja kwa ajili ya vipimo, ni mchezaji mzuri tulimfuatilia Gor Mahia, alicheza vizuri na hata kwenye mashindano ya SportPesa tulimuona pia,”alisema Bumbuli.

Bumbuli alisema anaamini ni mshambuliaji mzuri kwa sababu alionekana kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho akiwa na timu hiyo ya Kenya. Huo utakuwa ni usajili wa tano kwa Yanga tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo.

Tayari wamemsajili kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima kutoka AS Kigali, mshambuliaji Ditram Nchimbi kutoka Azam FC na Polisi Tanzania na beki wa JKT Tanzania, Adeyun Salehe na mchezaji wa zamani wa Biashara United, Tariq Seif.

Klabu hiyo ilianza kujiimarisha kwenye usajili baada ya baadhi ya wachezaji wake kuvunja mkataba ambao ni Sadney Urikhob na Juma Balinya.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

3 Comments

 • avatar
  mafuru mataba
  21/12/2019

  Comment. hakika ni usajili mzr tutarajie makubwa kutoka kwa wananchi.Yanga mbele nyuma mwiko

 • avatar
  Ndulu M.Malelemba
  22/12/2019

  Comment,Kuweni makini wachezaji wetu ilitufike mbali zaidi, Yanga mbele daima

 • avatar
  ELIA SAMSON
  23/12/2019

  Comment

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi