loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cruz: Waziri Mkuu mpya Cuba baada ya miaka 40

HATIMAYE nchi ya Cuba imempata Waziri Mkuu, baada ya kukaa miaka 40 bila mtu kushika nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, Rais Miguel Díaz-Canel amemteua Waziri Mkuu wa kwanza baada ya miaka 40, ambaye alikuwa Waziri wa Utalii, Manuel Marrero Cruz (56).

Nafasi ya Waziri Mkuu iliondolewa mwaka 1976 na kiongozi wa harakati za mapinduzi, Fidel Castro. Nafasi hiyo imerejeshwa kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Katiba mpya na kupitishwa mapema mwaka huu. Cruz (pichani), sasa atapaswa kutekeleza majukumu kadhaa ya kikatiba, ambayo awali yalikuwa yanafanywa na Rais.

“Mkuu wa Serikali atakuwa ni mkono wa kulia wa utawala wa rais wa jamhuri,” kilieleza kituo cha habari cha serikali cha Cubadebate.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema mabadiliko hayo ni kama mapambo tu, kwa kuwa Chama cha Kikomunisti cha Cuba na Jeshi, ndio vyombo vikuu viwili pekee vyenye maamuzi kwenye kisiwa hicho.

Uteuzi wa Marrero uliridhiwa kwa umoja katika Bunge la Kitaifa juzi. Marrero aliteuliwa na Fidel Castro kuwa Waziri wa Utalii mwaka 2004 na amefanya kazi kubwa ya kukuza sekta ya utalii nchini Cuba.

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania rasmi ametolewa kwa mkopo ...

foto
Mwandishi: HAVANA, Cuba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi