loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Vijana wa kujitolea JKT waitwa kupewa ajira

SERIKALI imetangaza ajira kwa vijana wote wenye shahada ya kwanza, waliohudhuria na kuhitimu mafunzo ya ‘t’ na kujitolea kufanya kazi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Sasa vijana hao wametakiwa kupeleka taarifa binafsi Ofisi ya Utumishi ndani ya siku 10 kuanzia jana. Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dk John Magufuli ya kutaka vijana wote wenye shahada ya kwanza, waliohudhuria na kuhitimu Operesheni Magufuli ambao wamejitolea kufanya kazi JKT, wapewe ajira serikalini.

Akizungumza jana jijini hapa, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema watakaonufaika na fursa hiyo ni wale waliojitolea na kuendelea kufanya kazi kwenye makambi ya JKT kwa kipindi cha miaka miwili.

“Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameamua kujitolea na kuendelea kufanya kazi kwenye makambi mbalimbali ya JKT kwa moyo na kujitolea, kwa kutambua mchango wao wa kujitolea Rais Magufuli alitoa maelekezo ya vijana hao wenye shahada ya kwanza waajiriwe na sisi tumeanza kulitekeleza hilo,” alisema Dk Ndumbaro.

Alisema vijana hao wanatakiwa kuwasilisha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora taarifa binafsi (CV), vyeti vya elimu, taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya JKT vilivyothibitishwa na JKT.

“Vijana hao wanatakiwa kuwasilisha taarifa binafsi, vyeti vya elimu na taaluma na vya kuhitimi JKT ili serikali iweze kuona namna ya kuwatumia vijana hao kwa kuwapata ajira katika maeneo mbalimbali ya serikalini,” alisema.

Aliongeza kuwa taarifa wanatakiwa kutuma kwa baruapepe ps@ utumishi.go.tz kuanzia jana hadi Januari 1, 2020. Alipoulizwa ni taaluma zipi ambazo vijana hao wataajiriwa, Dk Ndumbaro alisema tathimini ya awali ilionesha kuna takribani vijana 800 ambao wana sifa hizo na kuwa wote wenye sifa wataajiriwa.

“Kwa mwaka 2019/2020, serikali ilipanga kuajiri watumishi zaidi ya 40,000 ambazo tunatarajia kuanza kuzitoa mwezi Februari mwakani, katika nafasi hizo tumetoa fursa ya kuajiri vijana wote wenye shahada na waliojitolea JKT na wote tutawachukua maana walikuwa hawazidi 800 hivi,” alieleza.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

22 Comments

 • avatar
  Nassor .M.Songambele
  07/01/2020

  Ttz sina ajira na mtaj wa kujiajir mwenyewe nisaidien

 • avatar
  KELVIN ZAKARIA
  11/01/2020

  OMBI LANGU NI KUOMBA NAFASI YA KUJIUGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA (jkt) MWAKA 2020

 • avatar
  Emmanuel Philimoni
  20/01/2020

  Maombi yangu ni kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la kujenga TAIFA(JKT) naipenda nchi yangu TANZANIA nahaidi nitatumikia vema

 • avatar
  Emmanuel Philimoni
  20/01/2020

  Maombi yangu ni kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la kujenga TAIFA (JKT) naipenda nchi yangu naaidi nitaitumia vema nafasi hi (0786529960/0659872750)

 • avatar
  Robert Athanas
  09/02/2020

  Ombi, naomba nafasi ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa (jkt) 2020 natumaini nitatumikia vyema

 • avatar
  Mirashi kashimu
  12/02/2020

  Maombi yangu ni kujiunga na jeshi la kujenga taifa (JKT) natumaini nitatumikia vyema

 • avatar
  ADAMU RAJABU MGWEKO
  19/02/2020

  Kujiunga

 • avatar
  lineth A Revelian
  20/02/2020

  naomba nafasi JKT

 • avatar
  Mabula Msilikale
  01/03/2020

  Nahitaji kujiunga na jkt kwa kujitolea nikapate kulitumikia taifa langu

 • avatar
  Valerian theodemers swai
  01/03/2020

  Ombi langu naomba kujiunga na jkt 2020

 • avatar
  J.Rubeni
  01/03/2020

  Ombi langu nahitaji na ninaomba kujiunga na Jeshi la Tujenga Taifa Kwa mwaka 2020 ili niweze kushiriki vyema kuleta maendeleo katika Taifa langu

 • avatar
  evelius godifule
  03/03/2020

  wakuu ata me ninapenda kujiunga na jeshi ilo ili nilinde tanzania yang na Niko tayali kufanya chochot naomba munisaidie niweze kuitumikia nchi yang mungu ibaliki tz

 • avatar
  Anthony
  06/03/2020

  Amani na upendo wee! wazi

 • avatar
  James Francis
  18/03/2020

  Nimeishi kutamani Sana siku zote kutimiza ndoto zangu za kuwa mwanajeshi lakini bado sijafanikiwa moyo ninao ,Nia ninayo na vigezo ninavyo tafadhali nisaidie niipate nafasi ya jkt

 • avatar
  LADEN SAIDI NGOLOME
  18/03/2020

  naomba kujiunga na jeshi

 • avatar
  Recho Mwaigaga
  21/03/2020

  Je wale waliopo jkt alafu hawana stashad mnawasaidiaje?

 • avatar
  Amani Joshua
  29/03/2020

  Kwa mwaka huu (2020) Mimi nashauri , uandikishaji wa vijana ili kujiunga na jeshi, uanze mwezi July, kutokana na kuwepo kwa COVID-19...kwani kuna vijana wapo shule na vyuoni na wangetamani kujiunga Mara wamalizapo masomo yao.

 • avatar
  Daudi mwambene
  11/05/2020

  napenda sana kuwa mwanajeshi lakini kila nikifanya usahili nsishia ngazi ya mkoa najikuta tu sijachaguliwa mpaka naona nakaribia kupita umri uliopagwa napenda sana nije niwe mmoja wa watuliza amani duniani

 • avatar
  RADHIA ABEID MDOE
  03/06/2020

  kwa majina naitwa RADHIA ABEID MDOE nimemaliza elimu ya sekondari mwaka 2017. jaman mimi natamani sana na na penda pia kujiunga najeshi ila sasa najiuliza nitajiunga je na jeshi la kujenga taifa. kiufupi napenda sana na

 • avatar
  RADHIA ABEID MDOE
  03/06/2020

  Mimi ni binti mwenye umri wa mika 20 nimemaliza elimu ya ngu ya sekondari mwaka 2017 katika shule ya sekondari bumbuli. nakatika kipindi chote nilicho kua nyumbani nilijihusisha na vikosi mbalimbali kikiwemo kikosi cha scout na hatimaye kumaliza mafunzo ya scout. hivyo naomba msaada wakujiunga na jeshi la kujenga taifa kwani ni mojakati ya ndoto zangu. Napia nina vigezo vyote hivo nipenda kutoka moyoni nipotayari kwa lolote kwani napenda sana kutimiza ndoto zangu naomba kuwezeshwa. Natumaini ombi langu litafanyiwa kazi napatikana kupitia namba zifuatazo 0764296938/ 0718257361 nipo Tanga tanzania

 • avatar
  JAMES ALLY KAZUNGA
  09/06/2020

  Napenda kuuliz ivi nafas za jkt mwaka huu ztatoka kwel au? Mwene fununu yeyote anijuze

 • avatar
  RADHIA ABEID MDOE
  17/06/2020

  Habari zenu??? jamn ivi nafac zinatoka mwez ganiiiiii????

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi