loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

AfDB yamwaga mabilioni ujenzi barabara Mombasa- Bagamoyo

WATU zaidi ya milioni tatu katika nchi za Tanzania na Kenya, watanufaika na Euro milioni 345 kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kusaidia ujenzi wa barabara.

Barabara zitakazohusika ni za Mombasa-Lunga Lunga/Horohoro na Tanga-Pangani-Bagamoyo katika awamu ya kwanza, ikiwa ni asilimia 78.5 ya gharama zote ya ujenzi za Euro milioni 399.7. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na benki hiyo juzi, ilieleza kuwa Umoja wa Ulaya umechangia Euro milioni 30 ikiwa ni asilimia 7.7 ya gharama za mradi kwa serikali ya Kenya.

Barabara ni muhimu kwa mtandao wa usafiri Afrika Mashariki, inayounganisha Kenya na Tanzania ili kuwezesha wazalishaji, wenye viwanda na wafanyabiashara kusafirisha bidhaa kwa haraka na gharama nafuu. Pia wakulima na wavuvi, watanufaika na ujenzi wa barabara hizo kwa kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Mradi huu utanufaisha pia nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini zinazotegemea Bandari ya Mombasa kulifikia soko la dunia,” alisema Meneja wa Miundombinu, Sekta Binafsi na Viwanda katika benki hiyo, Hussein Iman.

Barabara hizo zitapunguza muda wa kusafirisha bidhaa, kuhamasisha biashara na muingiliano wa watu mipakani , kuvutia watalii, huku zikiunganisha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa na kukuza uchumi wa Pwani.

Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa barabara kilometa 175 ikiwamo kilometa 121 za barabara ya Mkanga-Pangani nchini Tanzania na Kilometa 54 za barabara ya Mombasa-Kilifi nchini Kenya.

Wiki hii, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ilitiana saini makubaliano ya Dola za Marekani milioni 440 na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano Japan (JICA) na serikali ya Kenya kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa daraja, linalounganisha kisiwa cha Mombasa na Likoni.

Bandari ya Mombasa ni ndefu Afrika katika Bahari ya Hindi. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara za Mombasa – Lunga Lunga/Horohoro na Tanga - Pangani – Bagamoyo kwa ujumla wa fedha zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 1.2 .

“Tuna imani kuwa tutafanya kazi pamoja kukamilisha suala hili muhimu na miradi mingine ijayo,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi