loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

TRA kuuza mali kwa mtandao

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua mfumo mpya wa uuzaji wa mali zake yakiwemo magari yanayokwama bandarini, jambo linaloifanya mamlaka hiyo kuachana na madalali, ambao kwa kipindi kirefu ndiyo walikuwa wakisimamia jukumu hilo.

Mnada huo huo kwa njia ya mtandao, unatarajiwa kufanyika rasmi kwa mara ya kwanza Januari 2, mwakani, na kuleta mabadiliko ya minada iliyokuwa ikifanywa na Kampuni za Yono, Majembe na zingine, ambazo huko nyuma ndizo zilikuwa zikifanya minada hiyo.

Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede amesema jijini Dar es Salaam kuwa, ujio wa mfumo huo, unaopatikana katika tovuti ya mamlaka hiyo, kwa kiasi kikubwa umelenga kutekeleza maagizo ya Rais Dk John Magufuli aliyemtaka kujenga taswira nzuri ya mamlaka hiyo wakati alipokuwa akimuapisha kushika nafasi hiyo.

Dk Mhede alisema kutokana na maagizo hayo, miongoni mwa hatua alizochukua ni kuzuia minada iliyokuwa ikifanywa kupitia madalali mbalimbali, ambapo tangu hatua hizo zichukuliwe mwezi mmoja uliopita, wamekuja na mfumo huo aliosema kuwa utasaidia kuiongezea mapato mamlaka hiyo.

Mbali na hilo, alisema kuanzishwa kwa mnada mtandao huo, pia kutazuia utapeli na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watu wasio waungwana, wakiwemo baadhi ya maofisa wake waliokuwa wakishirikiana kwa karibu na watu ambao hawakuwa madalali wala wanunuzi, bali walilenga kukwamisha minada hiyo.

Aidha, amesema kuanzishwa kwa mnada huo forodha wa kimtandao pia kutasaidia kuondoa vitendo vya kujirudia rudia kwa washiriki wa minada ambao hata hivyo alisema wengi wao siyo wanunuzi na kwamba mara kadhaa wamekuwa wakiingilia minada hiyo ili kukwamisha wanunuzi.

“Kwa sasa mnunuzi ataweza kufanya chaguo la bidhaa anayoitaka bila kuingiliwa na mtu yeyote, wanunuzi wote watapata fursa sawa ya kushindana kwa haki kwa ununuzi wa mali husika,” alisema.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo, ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

4 Comments

 • avatar
  ZAWADI SANGA
  30/12/2019

  Hongera sana TRA! Kwa ubunifu huo Wa mnada Wa kwa njia ya mtandaoni mtamfanya kila hudhuria.

 • avatar
  Theodory Mutayoba damian
  30/12/2019

  Ongereni Sana italeta uwazi,tulioko mikoani tutapata fursa

 • avatar
  ZAKAYO NGIMBUCHI
  19/01/2020

  Hongera TRA, kwa kuanza kutumia teknolojia ambayo ni nzuri zaidi na itaongeza mapato zaidi

 • avatar
  Kibadeni nzogela
  22/01/2020

  HONGERA SANA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi