loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EPZA kuvutia teknolojia viwandani

MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema inaendelea kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa, ili kukuza na kuendeleza wajasiriamali waitumie kukuza uchumi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alipozungumzia uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza kadi za kielekroniki cha DZ Cards Afrika, kilichopo katika Eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam.

Uwekezaji katika kiwanda hiki pekee kilichopo Afrika katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ni zaidi ya Sh bilioni 11.

Baadhi ya viwanda vilivyopo katika maeneo maalumu ya uwekezaji wa EPZ ni pamoja na viwanda vya nguo, vinavyochakata nafaka, vya kutengenezea vifungashio, vifaa vya ujenzi na vya bidhaa za ngozi.

Maziku alisema kuongezeka kwa mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza uchumi usiotumia fedha taslimu, ndio imefanya kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko ili kusambaza bidhaa zake katika bara lote la Afrika.

“Ongezeko la mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza matumizi Uchumi usiotumia pesa taslimu ndio imetoa msukumo mkubwa kwa wawekezaji wa kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko zaidi,” alisema Maziku.

Kiwanda cha DZ Cards Afrika kilianza uzalishaji miaka minne iliyopita na tangu wakati huo, kimepata wastani wa mauzo ya dola za Marekani milioni 2.9 (zaidi ya Sh bilioni 6.67).

Kiwanda hiki huzalisha kadi zenye viwango vya kimataifa zinazotumika katika kufanya miamala katika sekta mbali mbali za uchumi. Baadhi ya kadi hizo ni Mastercard na Visacard.

Maziku alisema kiwanda cha DZ Cards Afrika, kitakuwa na uwezo wa kuajiri zaidi ya watu 400 wakati uzalishaji ukiwa katika kiwango cha juu. Kwa sasa kinaajiri watu takribani 100.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi