loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera Polisi kudhibiti wahalifu

Watanzania wanaungana na wenzao duniani kote, kusherehekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka za Krsimasi na Mwaka Mpya.

Katika kipindi hiki cha sikukuu, watu wanastarehe na kujumuika na ndugu na jamaa zao katika shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, katika kipindi hiki pia huwa kuna ongezeko la vitendo vya vurugu na uhalifu kutoka makundi mengine mabaya.

Kutokana na hali hiyo, tunalipongeza Jeshi la Polisi kwa taarifa yao kuwa wamejipanga kuhakikisha kutakuwa na utulivu, amani na usalama wa hali ya juu wakati wote wa sikukuu hizi.

Kwa mfano, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Blasius Chitanda amesema wameimarisha ulinzi katika maeneo yote, ikiwemo kwenye mpaka wa Msumbiji na Tanzania, kwa sababu katika sikukuu hizi, kuna tabia ya baadhi ya watu kutoka Msumbiji huja Mtwara, kwa madai ya kusherehekea sikukuu hizi.

Kwamba sasa wanafanya doria kuanzia baharini ili kudhibiti wote wanaodhani wataingia Mtwara, kufanya uhalifu kupitia baharini mpaka mto Ruvuma. Chitanda anataka wananchi washerehekee sikukuu hizi kwa amani, kwani usalama upo wa kutosha kwenye maeneo yote, ikiwemo nyumba za ibada, fukwe za bahari na sehemu za starehe.

Anasisitiza kuwa mwenye uwezo wa kusherehekea kwa namna yoyote ile asherehekee, asiwe na shaka na usalama wake. Kwamba polisi wamejipanga vya kutosha na wana magari ya kutosha, mbwa wa kutosha na mashine za majini.

Tunalisifu pia Jeshi la Polisi kwa kujipanga kudhibiti wahalifu wanaotumia vyombo vya moto yakiwemo magari.

Taarifa ya Jeshi hilo ilieleza juzi kuwa wahalifu kamwe wasitegemee kuwa watapata nafasi ya kufanya vile wanavyotaka, wanapokuwa barabarani.

Badala yake, kutakuwa na ulinzi mkali maeneo yote ya barabara na lengo ni kuona Watanzania wanasherehekea sikukuu hizi bila matatizo yoyote.

Tunapongeza pia Jeshi la Polisi kwa kuwataka wamiliki wote wa kumbi za starehe, kuzingatia leseni zao za biashara, kwa kuhakikisha hakuna mikusanyiko ya watoto katika kumbi hizo yaani disco toto, kutokana na kutokuwepo umakini wa kutosha, juu ya idadi sahihi ya watoto wanaotakiwa kuingia ndani.

Hali kadhalika, tumevutiwa pia na kauli za viongozi wa dini za kuwahimiza Watanzania kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Mathalani, Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro, Telesphor Mkude akihubiri kwenye Ibada ya Krismasi, aliwaomba wananchi kusherehekea sikukuu zote hizi kwa amani, furaha na mshikamano na waendelee kudhibiti wahalifu, kwa kutoa taarifa polisi na vyombo vingine vya dola.

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), Jumanne ya wiki hii lilizindua ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi