loader
Picha

Jiji la Kigali lawa kivutio A. Mashariki

MOJA ya vivutio kikubwa nchini Rwanda sasa hivi ni jiji la Kigali ambalo ndilo makao makuu ya nchi hiyo.

Kutokana na kuvutia kwake, vyombo vya habari vya nchi hiyo ikiwamo televisheni, radio na magazeti vimekuwa vikilinadi jiji hilo kwa wageni.

Usafi na madhari nzuri ya mitaa iliyorembwa kwa taa za barabarani na muundo wa kisasa uliozingatia mipango miji na mazingira, ndivyo vitu ambavyo vinalifanya jiji hilo kushika nafasi za juu katika majiji bora barani Afrika, huku likiongoza kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jiji hilo hivi karibuni lilishika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa usafi na kuyapita majiji makubwa kama vile Cairo nchini Misri, Johannesburg nchini Afrika Kusini na Addis Ababa nchini Ethiopia.

Jiji la Kigali kwa mujibu wa mamlaka za jiji hilo, lina hoteli kubwa za kutosha za nyota tano, maeneo ya kihistoria yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya kuelimisha vizazi vya sasa na vijavyo pamoja na wageni ili kufahamu vizuri historia ya nchi hiyo.

Safu ya milima ya Musanze katika wilaya ya Musanze ni moja ya vitu vinavyopendezesha jiji la Kigali kwa asilimia kubwa. Kwa upande wa Kusini mwa jiji la Kigali kuna fukwe nzuri katika mwambao wa Ziwa Kivu. Mitaa mingi katika jiji la Kigali imewekwa lami na hivyo kuleta mvuto mkubwa katika jiji hilo linaloing’arisha Rwanda.

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

2 Comments

 • avatar
  good
  31/12/2019

  Commentgood

 • avatar
  uluru park
  07/01/2020

  Kigali huko mbeleni itashika nafasi ya kwanza Afrikaans mashariki kwa ukubwa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi