loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Matukio yaliyojiri Simba vs Yanga

KATIKA mchezo wa jana, kati ya Simba na Yanga kulishuhudia matukio matano kabla ya mchezo huo kuanza, Yanga kugoma kuingia kushuka katika basi lao.

-Yanga walifika Uwanja wa Taifa saa 9:25 alasiri, lakini wachezaji wao walikaa ndani ya gari kwa takriani dakika 20, huku baadhi ya makomandoo wakiwafukuza waandishi wa habari waliokuwa karibi na gari hilo. Ilikuwa tofauti kwa Simba, ambao wenyewe baada ya kufika uwanjani hapo walishuka katika gari lao na kuingia moja kwa moja katika chumba chao cha kubadilishia nguo.

SIMBA WAIFUNIKA YANGA

Kishangiliaji au kuchangamka, Simba waliifunika Yanga kabisa kabla ya kuanza mchezo huo. Dakika 15 kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, mashabiki wa Simba walionekana kuwa wenye wenye furaha kubwa baada ya hamshahamsha yao kubwa iliyowafunika kabisa wenzao wa Yanga, ambao walionekana kama vile hawataki kabisa kelele baada ya kutulia vitini kimya, wakisubiri mtanange kuanza. Pamoja na hilo, kwa mtazamo tu ilionekana mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi uwajani kushuhudia pambano hilo la watani wa jadi.

VURUGU KWENYE MAGETI

Mashabiki wa pande zote mbili walionekana kuwa na usongo mkubwa wa kuingia ndani ya uwanja kushuhudia mpambano huo, walikutana na changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa wakati mmoja, huku wasimamizi wa milangoni wakioneoneana kutojiandaa kupokea watu wengi kwa wakati mmoja.

Baadhi ya mashabiki waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kuwa, walikata tiketi lakini walizuiwa kuingia uwanjani baada ya mashabiki wa timu zote mbili kujaa uwanjani mapema na wengine kushindwa kupata sehemu ya kukaa, Wengine walikosa uvumilivu na kuamua kuondoka hata kabla mchezo haujaanza huku baadhi yao akilalamika wakidai mpangilio haukuwa mzuri na waliobaki wakijazana milangoni, walikutana na adha ya kufukuzwa na kutakiwa kukaa mbali kabisa.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Rahim Fadhili

2 Comments

 • avatar
  abdalah
  05/01/2020

  Comment

 • avatar
  Shambota willison
  08/01/2020

  Mpira ni mchezo wawazi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi