loader
Picha

Mafunzo ya mabalozi na maofisa wa ubalozi

Aidha, watu hao wawe watu wenye uelewa mzuri wa mambo ya nchi yao na nchi waliyopo; wawe wachapakazi na watu wa matokeo; wabunifu; wachambuzi; wazalendo, ujuzi wa mawasiliano; na pia, wawe na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko yanayotokea kila siku.

Kimsingi, sifa zao ni nyingi sana. Tangu Tanzania ilipopata uhuru, kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu uteuzi wa mabalozi na maofisa wa ubalozi. Wanazuoni wengi wanaamini kwamba, kwa kuwa uteuzi ulifanyika “kama apendavyo yeye”, ulitawaliwa na usiasa, undugu, urafiki, uchama na kulipa fadhila, badala ya matakwa ya diplomasia ya uchumi.

Tulishuhudia wakiteuliwa wastaafu, watoto wa viongozi, wanasiasa walioshindwa uchaguzi na mara nyingine kama njia ya kunyamazisha wanasiasa wakorofi. Wengi wa wateule hao, hawakuwa na uelewa wa diplomasia ya uchumi.

Matokeo yake, hatukufanikiwa sana katika eneo hilo. Tofauti na awamu zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa makini zaidi katika kuteua watekelezaji wa diplomasia ya uchumi. Tumeshuhudia wakiteuliwa vijana, wasomi na wazee waliobobea katika masuala mbalimbali ya kimataifa. Uteuzi wa Rais Magufuli umekuwa ukizingatia weledi na utendaji wa mtu zaidi ya kitu kingine chochote.

Aidha, Rais Magufuli ameonesha imani kubwa kwa mabalozi kwa kudhibiti safari holela za nje hivyo, kuchochea utendaji wao. Hii imepunguza gharama za maofisa wa ndani kwenda kutekeleza majukumu hayo.

Pia, mabalozi walitakiwa kuiwakilisha nchi kwa kuhudhuria mikutano itakayofanyika kwenye nchi walizopo au nchi jirani. Hali kadhalika, Rais Magufuli amekuwa akiwakumbusha mabalozi wajibu wao kwamba, hawakutumwa kwenda nje kunywa “wine,” bali kuhakikisha nchi inanufaika na uwepo wao huko.

Maana yake ni kwamba, mabalozi wanatakiwa wawe watu wa matokeo yaani, kila baada ya muda fulani waweze kueleza wameleta wawekezaji wangapi, wamepanuaje masoko kwa bidhaa zinazozalishwa Tanzania, wameleta watalii wangapi, wamesaidiaje kupata misaada na teknolojia ya kisasa.

Hapa kazi tu! Vile vile, Serikali ya Awamu ya Tano imefungua Ofisi za Ubalozi katika nchi za Israel, Cuba, Uturuki, Sudan Kusini, Algeria, Qatar na Korea Kusini. Hizi ni nchi za kimkakati ambazo Tanzania imekuwa ikinufaika na inaweza kunufaika zaidi (kwa biashara, uwekezaji, misaada, teknolojia, ulinzi na usalama na watalii) kwa kuwepo kwa ofisi za kibalozi katika nchi hizo.

MAFUNZO YA MABALOZI NA MAOFISA WA UBALOZI

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Mwaka 2014/15 ilionesha kwamba, kitengo cha diplomasia hakina wanadiplomasia wa kutosha na wenye ujuzi wa kutekeleza majukumu ya diplomasia ya uchumi. Ripoti hiyo ilioneesha pia kwamba, ofisi nyingi za ubalozi hazina wataalamu waliobobea kwenye uchumi na biashara, suala linalokwamisha utekelezaji wa diplomasia ya uchumi yenye mafanikio.

Japokuwa mabalozi na maofisa waandamizi wanapata mafunzo ya wiki moja kabla ya kuripoti vituo vyao vya kazi, mafunzo hayo hayatoshi. Tunahitaji mabalozi na maofisa wenye umahiri wa hali ya juu katika biashara, uwekezaji, utalii, misaada na mikopo, mazungumzo na kutangaza (branding) na kujenga taswira (image) ya nchi.

Wakati tunaingia mwaka wa tano wa Serikali ya Awamu ya Tano, ipo haja kuanzisha chuo maalumu (School of Diplomacy) kitakachowapika vilivyo mabalozi na maofisa waandamizi ili kuwajengea umahiri wa hali ya juu katika nyanja zote za diplomasia.

Tofauti ya chuo hicho na vyuo vingine ni kwamba, kitajishughulisha na kuwaandaa mabalozi na maofisa waandamizi kwa muda wa kutosha, siyo wiki moja. Mafunzo hayo yatajikita zaidi katika masuala ya kimataifa, sheria za kimataifa, diplomasia na hasa diplomasia ya uchumi. Ili kuwajengea maofisa umahiri unaotakiwa, chuo kitafundishwa na watalamu waliobobea katika fani hizo, mafunzo kwa vitendo/ mazoezi na ujenzi wa tabia zinazohitajika yatapewa kipaumbele.

Mbinu mbalimbali za kukabiliana na ujanja wa mataifa ya nje kuendelea kutunyonya, zitafundishwa. Mafunzo ya kutosha ni muhimu hasa kwa vile wapo mabalozi na maofisa waandamizi wanaochaguliwa, lakini hawana mafunzo na uzoefu wa kufanya kazi hiyo.

Mara nyingi maofisa hao wanachaguliwa kisha wanapewa mafunzo kidogo, halafu wanaachwa wakajifunze wakiwa kazini. Ni vema tukatambua kwamba, uwanja wa kimataifa si mahali salama pa majaribio kwa sababu wenzetu wanapeleka wataalamu waliobobea. Kwa maana hiyo, tukipeleka maofisa wa majaribio, tunaenda kushindwa!

KUENDELEZA UHUSIANO NA NCHI JIRANI

Pamoja na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitahada kubwa kuimarisha uhusiano na nchi za kigeni, jitihada kubwa zaidi zimefanyika kuimarisha uhusiano na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Kudhihirisha hilo, nchi chache ambazo Rais amezitembelea zipo kwenye jumuiya hizo. Aidha, kwenye mipaka ya nchi jirani vimeanzishwa vituo vya pamoja ili kuchochea mwingiliano wa watu na biashara.

Biashara na nchi jirani ina manufaa mengi kwa kuwa haina vikwazo vya umbali wa kijiografia, hivyo, kupunguza gharama za usafiri; vikwazo vya ubora na usafi kwa kuwa mahitaji na teknolojia yanafanana; vikwazo vya wingi wa bidhaa zinazohitajika; vikwazo vya kodi na visivyo vya kodi, vikwazo vya ushindani kibei; na kunakuwa na taratibu za kulinda masoko ndani ya jumuia.

Pia, serikali imekataa kuingia mikataba ya kibiashara (kama EPA) ya kinyonyaji na ambayo haina manufaa kwa taifa. Vile vile, serikali ya Tanzania pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zilikusudia kuzuia biashara ya mitumba kwa kuongeza kodi kwenye bidhaa hizo. Tukumbuke kwamba, mitumba ilianza kama misaada, ikakua ikawa biashara kubwa duniani, na sasa imekuwa kikwazo kwenye ujenzi wa viwanda.

UTAMBULISHO NA KUJENGA GTASWIRA YA NCHI

Kwa muda wote Rais Magufuli amekuwa akiitambulisha Tanzania kama nchi yenye utajiri mwingi inayostahili kutoa misaada, badala ya kuwa ombamba. Tanzania ina: aina nyingi za madini yakiwepo madini ya tanzanite yanayopatikana Tanzania tu; eneo kubwa lenye rutuba na linalofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali; mito, maziwa na ukanda bahari.

Inao pia utajiri wa hali ya hewa ya kuvutia; rasilimali watu ya kutosha; eneo kubwa lenye misitu; wanyama wengi wa kufugwa; ni ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya kitalii; ni nchi yenye amani na usalama na kijiografia ipo kimkakati kama lango la kuingilia nchi sita ambazo hazina bahari. Uwepo wa rasilimali zote hizo zinatoa fursa nyingi za uwekezaji.

Aidha, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi; ukuaji wa uchumi endelevu; ujenzi wa viwanda; kurekebisha sheria na mikataba ili nchi inufaike na rasilimali zake; ujenzi wa mazingira mazuri ya biashara, uwekezaji, utalii na misaada; utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kama ulivyoelezwa kwenye makala hii; na utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutumia fedha za ndani, vimeipa nchi heshima na kuijengea taswira nzuri kimataifa.

Dunia nzima inafahamu kuwa utekelezaji mbovu wa mambo ya ndani ndiyo adui namba moja wa maendeleo yetu. Na mataifa ya kigeni yanatumia udhaifu huo kujinufaisha!

HITIMISHO

Kwa kuwa masuala ya ndani ya kiuchumi ndiyo yanayoamua mafaniko ya diplomasia ya uchumi, Serikali ya Awamu ya Tano ilijikita zaidi kwenye kujenga mazingira mazuri ya ndani. Matokeo yake, nchi imeanza kunufaika, na kwa uhakika “yajayo yanafurahisha”!

UGONJWA wa Corona unaosababishwa na virusi vya ‘Covid 19’ ulianza ...

foto
Mwandishi: Prof. Kitojo Wetengere

1 Comments

  • avatar
    Brown
    09/01/2020

    Let me congratulate you for taking your time to talk about a new breed of Tanzanian ambassador abroad. It is sickening to and unbelievable to note that you can phone Tanzanian embassy in Pretoria for two weeks on the telephone registered on their website without anyone picking the phone. You can write million emails and no one bother. An embassy without a generator as a backup. When it happen to get them on phone they always tell you that our systems are down try after a week, and not tomorrow or later today. It's an embassy that in my whole life of visiting embassies for different services I never came across such deplorable attitudes towards work ethics. It seems no one has an answer to anything. Frontline workers are jokes I was astonished in my present an employee lifting the phone and put it down several times to discourage the phone calls and say in swahili inabidi niwashughulikie walio mbele yangu na sio wanaonisumbua na masimu yao ya mbali. The minister in charge need to develop a methodology to check the quality of services provided by their reps and if need be covertly.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi