loader
Picha

Museveni afanya matembezi jangwani

RAIS, Yoweri Museveni, ameanza matembezi ya siku sita jangwani, kama sehemu ya kumbukumbu ya jinsi vikosi alivyoviongoza kupambamba mwaka 1986 kunyakua madaraka mikononi mwa marais wa zamani wa nchi hiyo, Idi Amin na Milton Obote.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 1986, atakamilisha matembezi hayo katika mji wa Magharibi wa Birembo, eneo ambalo mapigano makali yalizuka kati ya vikosi vya waasi vikiongozwa na yeye mwenyewe na wanajeshi wa Obote, Junuari 10, mwaka huo.

Katibu mkuu wa mawasiliano ya Rais, Don Wanyama, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa: “Matembezi haya yanayoongozwa na Rais ni hatua ya kukumbuka yaliyopita ili kujivunia hali ilivyo sasa.”

“Matembezi haya yatadumu kwa wiki moja jangwani kupitia njia iliyopitiwa na wakombozi wa nchi wakiongozwa na Museveni.”

Wapinzani wake wamekosoa matembezi hayo, wakidai kuwa na mpango wa kujipatia umaarufu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao, ambapo Museveni anatarajiwa kugombea uraisi kwa muhula wa sita. Rais huyo wa Uganda anakabiliwa na upinzani kutoka kwa msanii wa zamani wa muziki na mwanasiasa, Bobi Wine, ambaye anajinadi kama mkombozi wa masikini.

FOMU za wagombea wanne kati ya 10 katika nafasi ya ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi