loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sadio Mane atangazwa mchezaji bora Afrika

MSHAMBULIAJI  wa timu Taifa ya Senegal na klabu ya Liverpool, Sadio Mane amechaguliwa kuwa mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2019, usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Mafanikio yanayotajwa kuwa sababu ya kutwaa tuzo hiyo, mbele ya wanandinga Riyad Mahrez na Mohamed Salah, ni kuiwezesha Liverpool kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) huku akiiongoza nchi yake kufika fainali za Mataifa ya Afrika, mwaka jana.

Mane anakuwa Msenegali wa pili kutwaa tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf ambaye alikuwa mchezaji bora kwa miaka miwili mfululizo, 2001 na 2002.

Mwaka huu, hafla ya kumtangaza mchezaji bora imefanyika katika jiji la Hurghada, nchini Misri.

Salah na Mane walikuwa wachezaji muhimu walioiwezesha Liverpool kutwaa Kombe la UEFA.

Msimu uliopita, Mane alifunga magoli 34, huku akitoa usaidizi katika magoli mengine 12 katika mechi 61 huku mpinzani mwenzake katika timu hiyo, Salah alifunga magoli 2 huku akitoa pasi za magoli 10 katika michezo 55.

Mane atangazwa mchezaji bora Afrika

Mashirika

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania rasmi ametolewa kwa mkopo ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi