loader
Picha

Jeshi la Iran lakiri kutungua ndege ya Ukraine 'kimakosa'

Jeshi la Iran limekiri usiku wa kuamkia leo Jumamosi kuwa liliiangusha ndege ya Ukraine na kuua abiria wote waliokuwemo ndani kimakosa, Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, limekinukuu kituo cha luninga cha Serikali ya Iran. 

Kituo hicho kimenukuliwa kikisema kuwa makosa hayo ya kibinadamu yalitokea pale ambapo ndege hiyo ilipokuwa ikikaribia maeneo nyeti la walinzi wa mapinduzi ya Iran. 

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa waliohusika watawajibishwa. 

Tukio la kuangushwa kwa ndege ya Ukraine International Airlines yenye usajili wa PS752 na kuua 176 lilitokea muda mfupi baada ya Iran kushambulia kambi mbili za kijeshi huko Iraq.

 

 

NDEGE ya abiria imemwagia mafuta shule kadhaa nchini Marekani wakati ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Nakizengi
    11/01/2020

    Jamani tuwe na roho ya huruma kuua watu wasio na hatia wanaouwawa ni wasio na hatia Fahari wanapigana nyasi ndio zinaumia watu tumeogope mungu mwenye kuua roho na mwili visasi visiangukie kwa raia wema

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi