loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

U17 yaikabili Burundi leo

TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, leo inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na timu ya Burundi katika mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India.

Mchezo huo ambao ni wa hatua ya awali unatarajiwa kuwa na ushindani kwa sababu timu hizi zinafahamiana na mara ya mwisho kukutana ni mwezi uliopita katika mashindano ya Cecafa yaliyofanyika nchini Uganda na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3. Baada ya mchezo wa leo timu hizi zitarudiana kati ya Januari 24, 25, na 26 Bujumbura, Burundi na mshindi atakutana na mshindi kati ya Uganda dhidi ya Ethiopia.

Akizungumza jana kocha wa timu hiyo Bakari Shime alisema wanatarajia kushinda mchezo kwani wanawafahamu vema washindani wao na hivi karibuni walikutana nao pia makosa yaliyowafanya kutoka sare wameyafanyia kazi.

“Burundi tunaifahamu vizuri kwani tulikuwa nayo katika mashindano ya Cecafa U17 yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Uganda, na tulitoka sare ya kufungana mabao 3-3, makosa yaliyojitokeza hadi wakasawazisha niliyaona na niliyafanyia kazi hivyo mchezo ujao tutafanya vizuri,” alisema Shime.

Pia Shime alisema wachezaji wote wako vizuri na wana ‘mechi fitinesi’ na hakuna majeruhi hivyo anaomba sapoti ya mashabiki ukizingatia hakuna kiingilio. Naye nahodha wa timu hiyo Irene Kisisa alisema wamejiandaa vya kutosha hivyo kesho (leo) wana kila sababu ya kushinda mchezo huo.

“Tumepata maandalizi mazuri na tumekaa kambini kwa muda mrefu hivyo tunaamini tutapata ushindi katika mchezo wetu ili tusonge mbele,” alisema Irene.

Pia aliwaomba Watanzania wajitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo na kuwapa nguvu w kwa kuwashangilia kwani hakuna kiingilio isipokuwa VIP B Sh 2000 na VIP A Sh 5000.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi